Thursday, February 21, 2013

WAJASIRIAMALI WADOGOWADOGO WAPEWA SEMINA YA PAPO KWA PAPO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa semina kwa baadhi ya kina mama wajasiriamali Mkoani Rukwa waliofika ofisini kwake kwa ajili ya msaada wa fikra na mtaji kuendeleza biashara zao ndogo ndogo. Kina mama ho wanaojishugulisha na bishara za kuuza karanga, mahindi ya kuchoma, mayai na mama lishe walipata somo kidogo juu ya kuendeleza biashara zao ambapo pia waliahidiwa kusaidiwa kuendeleza biashara zao. Miongoni mwa mafunzo waliyopewa ni utunzaji mzuri wa hesabu, usafi wa mwili, nguo na eneo la biashara, kujiwekea malengo pamoja na uchangamfu kwa wateja na ubunifu zaidi wa kuongezea thamani biashara zao. 
 
Injinia Stella Manyanya akitoa darasa kwa wajasiriamali hao wadogo wadogo akiamini kuwa hata wafanyabiashara wakubwa walianzia chini na hivyo kuwapa moyo kinamama hao kuwa mstari wa mbele kujikwamua kiuchumi.

Darasa likiendelea...zoezi hili la kuelimisha na kuwahamasisha kinamama wajasiriamali wadogo wadogo ni katika malengo waliojiwekea umoja wa wanawake mkoa wa Rukwa (RUWA) kuhakikisha mwanamke wa Rukwa anakua kiuchumi na kuondokana na umaskini. 
 
Mama Fausta Malenga mama wa watoto wa tano anajishughulisha na biashara ya uuuzaji mahindi ya kuchoma.
 
Maria Kilongozi Mjasiriamali biashara ya Mama Lishe
 
Magreth Otolo mjasiriamali biashara ya kuuza karanga...
 
Ester Sundu biashara ya kuuza mayai na machungwa....kwa ujumla wajasiriamali hao walimshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutojali udogo wao na kutumia muda wake kubadilishana nao mawazo juu ya shughuli ndogondogo wanazofanya, walisema kuwa wamefarijika sana na watayanyia kazi mawazo waliyopewa.

No comments:

Post a Comment