Friday, May 31, 2013

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA WAKIWA ZIARANI NCHINI JAPAN

IMG_3141
Rais Jakaya Kikwete akiambatana na mke wake Mama Salma tarehe 30. 5.2013 wakitembelea makumbusho ya karakana ya sayansi ya TOSHIBA iliyoko huko Kawasaki karibu na Tokyo nchini Japan inayohusika na utengenezaji wa injini za treni na vifaa vingine vye elektroniki wakiangalia laptop ya kwanza pamoja na calculator iliyotengenezwa na kampuni hiyo mwaka 1985. Rais Kikwete yupo nchini Japan kuhudhuria mkutano wa tano wa uhusiano wa kiuchumi kati ya Japan na Africa. 
 
 IMG_3147
Rais Jakaya Kikwete akiambatana na mke wake Mama Salma tarehe 30. 5.2013 wakitembelea makumbusho ya karakana ya sayansi ya TOSHIBA iliyoko huko Kawasaki karibu na Tokyo nchini Japan inayohusika na utengenezaji wa injini za treni na vifaa vingine vye elektroniki wakiangalia laptop ya kwanza pamoja na calculator iliyotengenezwa na kampuni hiyo mwaka 1985. Rais Kikwete yupo nchini Japan kuhudhuria mkutano wa tano wa uhusiano wa kiuchumi kati ya Japan na Africa. 
 
 IMG_3210
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Seneta Tetsuro Yano, Rais wa Association of African Economy and Development (AFRECO) wakati Mama Salma akifuatana na Rais Kikwete walipohudhuria kwenye chakula cha usiku (working dinner) kilichoandaliwa na seneta huyo pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan kuzungumzia uwekezaji wa Japan kwa nchi za Afrika . Working dinner hiyo ilifanyika huko Tokyo nchini Japan tarehe 30.5.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI

Thursday, May 23, 2013

DK. ASHA-ROSE MIGIRO ATAJA MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KILICHOFANYIKA DODOMA

1
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungunza na waandishi wa habari, jana katika ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Amezungumzia masuala mbalimbali yaliyojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichomalizika jana. (Picha na Bashir Nkoromo)
 
TAARIFA KAMILI ALIYOTOA DKT. MIGIRO
 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilifanya kikao chake cha kawaida mjini Dodoma Mei 21, 2013 chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ilijadili na kutafakari masuala mbali mbali yanayohusu Uchumi, Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Taifa.


MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI


Migogoro ya wakulima na wafugaji imekuwa mingi na imeenea sana katika taifa letu. Migogoro hii inatokana na sababu nyingi: mabadiliko ya tabia nchi; ongezeko la idadi ya watu na mifugo. Kamati Kuu inasikitishwa na kuendelea kwa migogoro hii ambayo imekuwa tishio la amani na usalama katika jamii, na pia kusababisha wakulima kupata hasara baada ya mazao yao kuliwa na mifugo. Tumeishuhudia migogoro hii mkoani Morogoro hivi karibuni, katika ziara ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana na imeripotiwa katika maeneo mengine ya nchi yetu.Kamati Kuu inaiagiza Serikali kuishughulikia na kuitafutia ufumbuzi wa kudumu migogoro hii. Kamati Kuu inaiagiza Serikali kuharakisha zoezi la kutenga maeneo kwa ajili ya wakulima na wafugaji na kujenga miundombinu ya malisho, maji, na majosho ili kuwezesha wafugaji kutohamahama na mifugo yao.

KULINDA HIFADHI
Kamati Kuu imezungumzia suala la mahusiano kati ya Hifadhi za taifa, wafugaji na wananchi waishio katika vijiji vinavyozunguka Hifadhi hizo. Kamati Kuu inatambua umuhimu wa Hifadhi kwa manufaa ya taifa letu na vizazi vijavyo. Inasisitiza msimamo wake wa kuzilinda Hifadhi za taifa sanjari na kuanzisha na kuendeleza mahusiano hayo.


Kamati Kuu inaiagiza Serikali kuwashirikisha wananchi katika kutenga maeneo ya Hifadhi, kulinda maeneo ya wanyama pori na kutenga maeneo ya malisho ili kuondosha migogoro isiyo ya lazima katika maeneo yanayozunguka Hifadhi.

ZAO LA KOROSHO
Kamati Kuu ilijadili matatizo yanayolikabili zao la korosho ambayo ni: kuyumba kwa bei ya korosho, malipo ya wakulima kuchelewa, tozo nyingi wanazolipishwa wakulima na udhaifu wa baadhi ya vyama vya ushirika.

Tatizo hili limedumu kwa muda mrefu na linastahili kushughulikiwa kwa njia ya kipekee.Kwa kutambua kwamba wapo baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali, viongozi wa vyama vya ushirika na wafanyabiashara binafsi wanaochangia katika kuendeleza matatizo yanayowakabili wakulima wa korosho:

Kamati Kuu inatamka kwamba hali hii haivumiliki. Kamati Kuu inaitaka Serikali kukaa na wadau wote na kuchukua hatua zitakazotoa ufumbuzi wa kudumu wa matatizo haya kwa zao la korosho. Kamati Kuu pia inaitaka Serikali kuwachukulia hatua za kisheria hao wote wanaochangia kuendelea kwa matatizo haya kwa wakulima wa korosho.

MIGOGORO YA KIDINI
Kamati Kuu imepokea taarifa ya namna migogoro ya kidini inavyoshughulikiwa na hatua zinazochukuliwa. Kamati Kuu inaipongeza Serikali na vyombo vya dola kwa namna inavyoendelea kukabiliana na wahalifu wanaotumia mgongo wa dini kuanzisha vurugu na uvunjifu wa amani katika nchi yetu. Kamati Kuu inatoa mwito kwa Watanzania kukataa vitendo vyote vinavyochochea migogoro ya kidini; wananchi wajihadhari na watu waovu wenye nia mbaya ya kuligawa taifa letu.


Pamoja na jitihada za vyombo vya dola hadi sasa, Kamati Kuu inaitaka Serikali iandae mkakati wa kuzuia migogoro ya kidini kabla haijajitokeza.
MAKAMPUNI NA VIWANDA VILIVYOBINAFSISHWA
Kamati Kuu imetafakari hali ya viwanda hivi. Ni muongo mmoja umepita tangu ubinafsishaji ulipokamilika. Kuuzwa kwa mashirika na viwanda vya umma kwa watu na makampuni binafsi kumekuwa na matokeo ya aina mbili: yako yale yaliyobinafsishwa na yakawa na maendeleo mazuri na kuchangia uchumi wa Taifa. Na yako ambayo yanaendeshwa kwa kiwango cha chini au yamefungwa.


Kamati Kuu inasikitishwa na hali hii, kwani viwanda vilivyofungwa ni vile vilivyokuwa vikifanya kazi muhimu ya uzalishaji.

Viwanda hivi ni vya korosho, usindikaji wa pamba, mafuta ya kula, viwanda vya mazao ya ngozi, na vinginevyo. Hali hii inalikosesha Taifa fursa za ajira, kukua kwa mapato, kuimarika kwa uzalishaji na kuongezeka kwa uuzaji wa bidhaa zilizosindikwa na kuzalishwa nchini.

Imedhihirika kuwa wafanyabiashara waliochukua viwanda hivyo ndiyo hao hao wanaofanya biashara ya kununua mazao ya kilimo na mifugo na kuuza nje kama bidhaa ghafi, wakati huo huo wakiwa wamevifunga viwanda hivi.

Kamati Kuu inaiagiza Serikali kufanya tathmini ya viwanda vilivyobinafsishwa ili kuvitambua vile vilivyofungwa, na kuwataka waliouziwa wavifungue na iwapo watashindwa kutimiza masharti yaliyowekwa, Serikali iandae utaratibu wa kuwapa watu wenye uwezo wa kuviendesha.

WAKULIMA WADOGO WA MIWA -
Kumekuwapo na migogoro ya muda mrefu kati ya wakulima wadogo wa miwa na Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa mkoani Morogoro. Matatizo haya yameshughulikiwa na watendaji mbalimbali bila ya kupatikana kwa ufumbuzi wa kudumu.


Kamati Kuu inaiagiza Serikali kuushughulikia mgogoro huu na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu matatizo ya wakulima wadogo wa miwa haraka iwezekanavyo.

PEMBEJEO ZA KILIMO.

Chama kimejiridhisha kuwa suala la utoaji wa pembejeo za kilimo ni zuri na lenye mafanikio. Hata hivyo Kamati Kuu imepokea taarifa kuhusu matatizo yanayohusiana na usambazaji wa mbolea ya ruzuku.

Kwa baadhi ya maeneo mbolea ya ruzuku imekuwa ikitolewa kwa watu wasiohusika na wakati mwingine walanguzi wamekuwa wakiingilia kati ili kujinufaisha nayo.

Kamati Kuu inaiagiza Serikali kusimamia kwa umakini na kutafuta utaratibu bora zaidi na wenye tija wa kuwafikishia wakulima mbolea, kwa wakati na kwa uhakika.


MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI.
 Kamati Kuu imepokea taarifa na kuipongeza Serikali kwa kutayarisha mpango kabambe wa ujenzi wa nyumba za watumishi wake. Mpango huu utatoa fursa kwa wafanyakazi ya kupata mikopo yenye masharti nafuu na hivyo kuwawezesha kuwa na makaazi yenye uhakika.

MWISHO:
Kamati Kuu imeitaka Serikali kuwasilisha utekelezaji wa maagizo haya mara kwa mara.


IMETOLEWA NA:

Asha-Rose Migiro,
Katibu WA NEC – Siasa Na Uhusiano wa Kimataifa,
Mei 22, Dodoma.

Wednesday, May 22, 2013

RAIS KIKWETE ASISITIZA RASILIMALI INAYOPATIKANA POPOTE NCHINI NI YA WATANZANIA WOTE, WANAOSABABISHA VURUGU MTWARA KUSAKWA NA KUWAJIBISHWA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekemea vikali vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Akizungumza katika eneo la Kizota mkoani Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali.

Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote.

“Hivi watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo.

“Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.” Alisema kwa msisitizo.

mtwara-ambulance-manispaa-motoGari ya kubebea wagonjwa Ambulance inaonekana kuteketea kwa moto baada ya kuchomwa katika vurugu zilizoripotiwa kutokea mara kadhaa mkoani Mtwara.
mtwara-vurugu
Moto ukiwa umeshawashwa baadhi ya maeneo ya Mtwara na kusababisha uharibifu wa mali.
mtwara-vurugu-magari-yachomwa-moto
Magari yanayosemekana kuwa ya Halmashauri yakiwa yamechomwa moto na wananchi wa Mtwara.
ofisi-moto-mtwara
Majengo yanayotajwa kuwa ofisi zimechomwa moto
Vurugu hizi zimetokea siku chache baada ya Wizara ya Nishati na Madini kusema kuwa bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam na leo hii Wananchi wa Mtwara wacharuka na kuanzisha vurugu!
Tukio hili liliendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa Bungeni.

WORKSHOP

 
BTG Group LTD ( www.btgforafrica.com ) is holding a one-day workshop titled: Leadership Skills for the Global Marketplace. Attendees will receive training in:

Business Negotiations
Cultural Intelligence
Leadership Values
Cyber Security Management

The quality of your business's employees is directly related to the success of your organization. The strategies and topics covered during this workshop will give your employees the edge in advancing your business.

Date: Thursday 6, June 2013
Time: 9AM - 4PM
Location: Holiday Inn, Dar es Salaam, City Centre

For registration and details, please visit:
www.btgforafrica.com/workshop

We hope to see you there!

Friday, May 17, 2013

PSPF MKOANI RUKWA YATOA SOMO KWA WADAU JUU YA UMUHIMU WA MFUKO HUO KATIKA KUHITIMISHA WIKI YA HIFADHI YA JAMII NCHINI

Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akitoa somo kwa wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa (Rukwa Teacher's College) juu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa Umma. Semina hiyo imeenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini iliyofanyika kitaifa Mkoani Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza kilele cha maadhimisho hayo leo tarehe 17.05.213.
 
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakimsikiliza mtoa mada kwa umakini mkubwa. Wahitimu hao ni sehemu ya wadau wakubwa wa baadae wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.
 
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akiendelea na kutoa mada alizoandaa kwa wahitimu hao juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wenye mafao mbalimbali.
 

Malipo ya uzeeni, Malipo ya ulemavu, Malipo ya mirathi, Malipo ya wategemezi, na Malipo ya mazishi ni sehemu ya mafao muhimu yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa umma. 
 

Wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakionekana kukolea na mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
 
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akiagana na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu chuoni hapo baada semina ya shughuli na mafao muhimu yanayotolewa na mfuko wa PSPF nchini.

Thursday, May 16, 2013

JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE OTHMAN AKIWA ZIARANI MKOANI RUKWA AONANA NA UONGOZI WA MKOA HUO LEO

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Rukwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo mapema leo tarehe 16.05.2013 ambapo alizungumzia mambo kadhaa muhimu kuhusu sekta ya mahakama nchini na umuhimu wa kuboresha amani, ulinzi na usalama katika taifa unaokwenda sambamba na kuweka msukumo wa maendeleo nchini.
 
Jaji Mkuu akifafanua jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
 
Jaji Mkuu akiongoza kikao hicho kilichojumuisha msafara wake na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Rukwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo (aliyesimama) Moshi Chang'a akizungumza katika kikao hicho.
 
TAARIFA YA MKOA WA RUKWA KWA JAJI MKUU LEO TAREHE 16 MEI, 2013

Wednesday, May 8, 2013

SIKU YA WAUGUZI KITAIFA KUFANYIKA MKOANI RUKWA TAREHE 10-12 MEI 2013, WAZIRI WA AFYA DKT. HUSSEIN MWINYI KUWA MGENI RASMI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea na wananchi kupitia vyombo vya habari kutoa taarifa juu ya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani itakayofanyika kitaifa Mkoani Rukwa kuanzia tarehe 10 hadi 12 ambapo mgeni rasmi anategemewa kuwa Waziri wa Afya Dkt. Hussein Mwinyi. Soma zaidi juu ya siku hiyo hapo chini baada ya picha.

 
Timu ya wauguzi kutoka Hospitali kuu ya Mkoa wa Rukwa ikiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kushoto na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Alhaj Salum Mohammed Chima kulia wakati wa kutoa taarifa ya maandalizi ya siku hiyo kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.
 

Thursday, May 2, 2013

HOTUBA YA RAIS KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI 2013 JIJINI MBEYA


SERIKALI YATANGAZA KUPUNGUZA KODI KATIKA MISHAHARA ...........................................................

Wafanyakazi nchini watapata nafuu kimapato, pale Serikali itakapoanza kutekeleza azma yake ya kupunguza kodi kwenye mishahara (PAYE) wiki mbili zijazo.
Rais Jakaya Kikwete, jana aliashiria hivyo baada ya kutangaza punguzo la PAYE, kwa lengo la kupunguza mzigo wa ugumu wa maisha kwa mfanyakazi.
 

 
Alitangaza hatua hiyo alipohutubia wananchi jana katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, yaliyofanyika kitaifa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya na kutangazwa moja kwa moja na vyombo vya habari.

SIKUKUU YA WAFANYAKAZI (MEI MOSI) MKOANI RUKWA ILIVYOSHEREHEKEWA WILAYANI NKASI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali pamoja na wadau mbali mbalimbali na wafanyakazi wakiimba wimbo wa wafanyakazi maarufu kama "Solidarity Forever" Katika viwanja vya sabasaba mjini Namanyere Wilayani Nkasi zilipofanyika sherehe hizo kimkoa jana. Kauli mbiu ya sherehe hizo za Mei Mosi mwaka huu ni "KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA NA HAKI KWA TABAKA LWA WAFANYAKAZI"
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta wakiangalia maonesho mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na wafanyakazi wa sekta mbalimbali katika kufanikisha sherehe za Mei Mosi Wilayani Nkasi zilizofanyika huko kimkoa jana.
 

Maonesho ya wafanyakazi wa Serikali na Sekta binafsi kwa vitendo ilinogesha sherehe hizo.
 
Maandamano ya wafanyakazi na mabango yenye jumbe mbalimbali ilikuwa sehemu ya maadhimisho hayo. Kauli Mbiu ya sherehe hizo kitaifa ilikuwa "KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA NA HAKI KWA TABAKA LWA WAFANYAKAZI"
 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashala wakiangalia maonesho mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na wafanyakazi wa sekta mbalimbali katika kufanikisha sherehe za Mei Mosi Wilayani Nkasi zilizofanyika huko kimkoa jana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitetea jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika kimkoa Wilayani humo jana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi cheti na zawadi mmoja ya wafanyakazi bora wa mwaka 2012/2013 katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Elvira Malema ambaye Sekretari wa Mkuu  huyo wa Mkoa jana katika uwanja wa sabasaba Mjini Namanyere Wilayani Nkasi. Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Iddi Hassan Kimanta.
 
Michezo mbali mbali ya mpira wa miguu na netiboli pia ilifanyika ikiwa ni kuhamasisha michezo kwa wafanyakazi kwa ajili ya kuboresha afya zao kazini na kazi zao kwa ujumla. Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa salam za Mei Mosi kwa wachezaji wa timu za Veteran Sumbawanga na Namanyere Nkasi kabla ya kuanza kwa mpambano, timu hizo zilitoa sare 1-1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta.