Friday, May 17, 2013

PSPF MKOANI RUKWA YATOA SOMO KWA WADAU JUU YA UMUHIMU WA MFUKO HUO KATIKA KUHITIMISHA WIKI YA HIFADHI YA JAMII NCHINI

Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akitoa somo kwa wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa (Rukwa Teacher's College) juu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo pamoja na mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa Umma. Semina hiyo imeenda sambamba na maadhimisho ya wiki ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini iliyofanyika kitaifa Mkoani Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza kilele cha maadhimisho hayo leo tarehe 17.05.213.
 
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakimsikiliza mtoa mada kwa umakini mkubwa. Wahitimu hao ni sehemu ya wadau wakubwa wa baadae wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.
 
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akiendelea na kutoa mada alizoandaa kwa wahitimu hao juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko huo wenye mafao mbalimbali.
 

Malipo ya uzeeni, Malipo ya ulemavu, Malipo ya mirathi, Malipo ya wategemezi, na Malipo ya mazishi ni sehemu ya mafao muhimu yanayotolewa na mfuko huo kwa watumishi wa umma. 
 

Wahitimu wa mafunzo ya ualimu katika chuo cha ualimu Rukwa wakionekana kukolea na mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
 
Afisa Mfawidhi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Mkoa wa Rukwa Ndugu Paul Mbijima akiagana na baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu chuoni hapo baada semina ya shughuli na mafao muhimu yanayotolewa na mfuko wa PSPF nchini.

No comments:

Post a Comment