Wednesday, May 22, 2013

RAIS KIKWETE ASISITIZA RASILIMALI INAYOPATIKANA POPOTE NCHINI NI YA WATANZANIA WOTE, WANAOSABABISHA VURUGU MTWARA KUSAKWA NA KUWAJIBISHWA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekemea vikali vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara baada ya kusomwa bungeni kwa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Akizungumza katika eneo la Kizota mkoani Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali.

Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote.

“Hivi watu wa Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo.

“Tutawasaka hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.” Alisema kwa msisitizo.

mtwara-ambulance-manispaa-motoGari ya kubebea wagonjwa Ambulance inaonekana kuteketea kwa moto baada ya kuchomwa katika vurugu zilizoripotiwa kutokea mara kadhaa mkoani Mtwara.
mtwara-vurugu
Moto ukiwa umeshawashwa baadhi ya maeneo ya Mtwara na kusababisha uharibifu wa mali.
mtwara-vurugu-magari-yachomwa-moto
Magari yanayosemekana kuwa ya Halmashauri yakiwa yamechomwa moto na wananchi wa Mtwara.
ofisi-moto-mtwara
Majengo yanayotajwa kuwa ofisi zimechomwa moto
Vurugu hizi zimetokea siku chache baada ya Wizara ya Nishati na Madini kusema kuwa bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam na leo hii Wananchi wa Mtwara wacharuka na kuanzisha vurugu!
Tukio hili liliendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa Bungeni.

No comments:

Post a Comment