Thursday, May 2, 2013

SIKUKUU YA WAFANYAKAZI (MEI MOSI) MKOANI RUKWA ILIVYOSHEREHEKEWA WILAYANI NKASI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali pamoja na wadau mbali mbalimbali na wafanyakazi wakiimba wimbo wa wafanyakazi maarufu kama "Solidarity Forever" Katika viwanja vya sabasaba mjini Namanyere Wilayani Nkasi zilipofanyika sherehe hizo kimkoa jana. Kauli mbiu ya sherehe hizo za Mei Mosi mwaka huu ni "KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA NA HAKI KWA TABAKA LWA WAFANYAKAZI"
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta wakiangalia maonesho mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na wafanyakazi wa sekta mbalimbali katika kufanikisha sherehe za Mei Mosi Wilayani Nkasi zilizofanyika huko kimkoa jana.
 

Maonesho ya wafanyakazi wa Serikali na Sekta binafsi kwa vitendo ilinogesha sherehe hizo.
 
Maandamano ya wafanyakazi na mabango yenye jumbe mbalimbali ilikuwa sehemu ya maadhimisho hayo. Kauli Mbiu ya sherehe hizo kitaifa ilikuwa "KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA NA HAKI KWA TABAKA LWA WAFANYAKAZI"
 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashala wakiangalia maonesho mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na wafanyakazi wa sekta mbalimbali katika kufanikisha sherehe za Mei Mosi Wilayani Nkasi zilizofanyika huko kimkoa jana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitetea jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika kimkoa Wilayani humo jana.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi cheti na zawadi mmoja ya wafanyakazi bora wa mwaka 2012/2013 katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Elvira Malema ambaye Sekretari wa Mkuu  huyo wa Mkoa jana katika uwanja wa sabasaba Mjini Namanyere Wilayani Nkasi. Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Iddi Hassan Kimanta.
 
Michezo mbali mbali ya mpira wa miguu na netiboli pia ilifanyika ikiwa ni kuhamasisha michezo kwa wafanyakazi kwa ajili ya kuboresha afya zao kazini na kazi zao kwa ujumla. Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa salam za Mei Mosi kwa wachezaji wa timu za Veteran Sumbawanga na Namanyere Nkasi kabla ya kuanza kwa mpambano, timu hizo zilitoa sare 1-1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta.

No comments:

Post a Comment