Tuesday, August 6, 2013

TASO YAIVIMBIA SERIKALI YAGOMA KUAHIRISHA SHEREHE ZA NANENANE KUPISHA SIKUKUU YA IDDI

Mwenyekiti wa TASO Kanda ya nyanda za juu Kusini Kepten mstaafu Nkoswe.

 
Siku chache zikiwa zimebaki ili kufikia kilele cha maadhimisho ya s kumeibuka mgongano baina ya Chama cha wakulima (TASO) na serikali kuhusu maadhimisho hayo yafanyike Agosti 7 au 8, mwaka huu.

 
Mgongano huo umekuja baada ya serikali kutaka maadhimisho hayo yafanyike Agosti 7 mwaka huu huku chama cha wakulima kikiweka msimamo wake wa kusherehekea maadhimisho hayo agosti, 8 mwaka huu .

 
Akizungumza jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale Mwenyekiti wa Chama cha wakulima (TASO) kanda ya nyanda za juu kusini,Kapten Mstaafu Noel Nkoswe wakati wa majumuisho na waandishi wa habari baada ya kuibuka vuta nikuvute na serikali kuhusu kilelele cha maadhimisho hayo ya wakulima.

 
Kapten Nkoswe amesema kuwa wao kama chama cha wakulima msimamo wao upo pale pale wa sherehe hiyo ya wakulima kufanyika Agosti 8 mwaka huu kama ilivyopangwa kila mwaka.

Amesema Wakulima wao lazima l washerekee sikukuu yao kama kawaida hivyo mpango wa kubadilisha tarehe haupo ambapo chama hicho kwa msimao wake kitafanya tarehe 8 na zawadi za wakulima kutolewa agosti 8 kama ilivyo pangwa.

 
Kapten mstaafu Nkoswe amesema mwenyekiti wa TASO taifa aliyemtaja kwa jina moja amemwelekeza kuwa maadhimisho ya kilele cha sikukuu hiyo yatafanyika kitaifa katika kanda ya kati Dodoma Agosti 7 mwaka huu ambapo katika kanda zingine zitafanya kama kawaida Agosti 8 mwaka huu.

 
Hata hivyo kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.Christine Ishengoma amesema kuwa wamepokea barua ya serikali inayotaarifu sherehe za kilele cha nane nane zifanyike Agosti 7 mwaka huu kutokana na sikukuu ya Idd kuwa agosti 8 mwaka huu .

 
Hata hivyo katika barua iliyotumwa na wizara ya kilimo chakula na ushirika yenye kumbu kumbu namba AE 18/196/01 ya julai 30 mwaka huu kwenda kwa waziri wa nchi sera uratibu na bunge ofisi ya waziri mkuu iliyoandikwa na waziri wa kilimo na chakula Eng Christopher Chiza na nakala kwa wakuu wa mikoa yote minne ya kanda ya nyanda za juu kusini.

 
Aidha nakala ya barua hyo iliyotumwa kwa katibu mtendaji Taifa imesema kuwa sherehe za kilele cha nane nane imeamliwa zifanyike Agosti 7 mwaka huu kutokana na mwingiliano wa sikukuu ya Idd ambapo Waziri wa nchi Mh.William Lukuvi atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.

 
NA mbeya Yetu Blog.

No comments:

Post a Comment