Sunday, September 29, 2013

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AWASILI MKOANI RUKWA KUSHIRIKI IJITIMAI YA KIMATAIFA

Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya aliopowasili leo tarehe 29 Septemba 2013 katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga kwa ajili kushiriki na kufunga Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika Mkoani Rukwa. Ijitimai ni Semina ya kiislam inayolenga kuihamasisha jamii kumcha Mungu kwa kufanya matendo mema na kuacha maovu na machafu.

Kiongozi wa maandalizi ya Ijitimai ya kitaifa na kimataifa inayofanyika Mkoani Rukwa Amir Ali Jumanne akimtambulisha Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam walioshiriki katika maandalizi ya Ijitimai. 
 
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini CCM, Aeishi Hillal akiteja jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima wakati wa mapokezi ya Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimsomea Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad taarifa ya Mkoa wa Rukwa katika Ikulu ndogo ya Sumbawanga.
 
Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akizungumza mara baada ya kusomewa taarifa ya Mkoa wa Rukwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya. Katika mazungumzo yake ameshukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuupongeza Mkoa wa Rukwa kwa uzalishaji mkubwa wa chakula nchini ambapo ameutaka uongozi wa Mkoa kujikita zaidi kutafuta masoko ya mazao yanayozalishwa na wakulima. 
 
Ameutaka pia uongozi wa Mkoa kulipa kipaombele suala la usalama akitolea mfano yaliyotokea nchini kenya na kuvitaka vyombo vya dola kuimarisha uhusiano na wanachi katika kuboresha taarifa za ulinzi shirikishi. Aliwaasa pia wanachi kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo nchini kwa kuweka pembeni tofauti zao za kidini na kusaidia kutoa taarifa inayoashiria uvunjifu wa amani kwa vyombo vya dola .
 
Akizungumzia kongamano la uwekezaji lililofanyika Mkoani Rukwa mwaka jana ameutaka uongozi wa Mkoa kujitangaza zaidi katika fursa zinazopatikana za uwekezaji na kufuatilia wawekezaji waliotoa ahadi za kuwekeza Mkoani Rukwa na kuwawekea mazingira mazuri ya kuwekeza. 
 
Baadhi ya viongozi wa dini na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar walioongozana na Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad. Katikati ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Said Ali Mbarouk. Wengine ni Chief Kadhi wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis na Imam Sheikh Mziwanda Ngwali.

Saturday, September 28, 2013

TAASISI YA BENJAMIN WILLIAM MKAPA HIV/AIDS YAKABIDHI NYUMBA 20 ZA WATUMISHI WA IDARA YA AFYA MKOANI RUKWA


Afsa Mtendaji Mkuu Mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Bi. Elena Senkoro akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya cheti cha makabidhiano ya nyumba 20 za watumishi wa idara ya afya zilizojengwa Mkoani Rukwa na mfuko huo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria leo tarehe 28 Septemba 20113 katika kijiji cha Chipu pembeni kidogo ya Manispaa ya Sumbawanga. Anaeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt. Herman Lupogo.
 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizindua rasmi moja ya nyumba 20 za watumishi wa idara ya afya katika kijiji cha Chipu baada ya kukabidhiwa rasmi na taasisi ya Benjamin William Mkapa leo tarehe 28 Septemba 2013.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa katika picha ya pamoja na mtumishi wa idara ya afya katika zahanati ya Chipu (kulia) ambaye ataishi katika nyumba hii iliyojengwa na mfuko wa taasisi ya Benjamin William Mkapa. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe na Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Dkt. Herman Lupogo.
 
Moja ya nyumba 20 zilizojengwa na taasisi hiyo iliyopo Ntendo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
 

Afisa Mtendaji Mkuu Mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Bi. Elena Senkoro akielezea miradi mbalimbali ya taasisi hiyo katika kusaidia jamii ya watanzania.
 

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitambulisha baadhi ya wageni katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano.
 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akipanda mti wa kumbukumbu katika hafla hiyo ya makabidhiano.
 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipanda mti wa kumbukumbu baada ya makabidhiano ya nyumba 20 zilizojengwa na mfuko wa taasisi ya Benjamin William Mkapa Mkoani Rukwa. 
 
Mbunge wa Jimbo la Sumbwanga Mjini CCM, Aeshi Hillal akipanda mti wa kumbukumbu.
 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akimnong'oneza jambo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya muda mfupi baada ya makabidhiano ya nyumba hizo.
 
Picha ya Pamoja.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Afsa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa Bi. Elena Senkoro  cheti cha shukurani na kutambua mchango wao katika ujenzi wa nyumba 20 za watumishi wa idara ya afya Mkoani Rukwa.


Friday, September 27, 2013

SERIKALI YA MKOA WA RUKWA IKIONGOZWA NA MKUU WA WILAYA YA KALAMBO YAWATEMBELEA WAHANGA WA AJALI YA BOTI ILIYOUA 13 NA WENGINE 15 KUNUSURIKA KATIKA KIJIJI CHA KIPWA MWAMBAO MWA ZIWA TANGANYIKA

 Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akitoa baadhi ya maelekezo kwa nahodha wa Boti mara baada ya kuanza safari kuelekea katika Kijiji cha Kipwa mwambao mwa ziwa Tanganyika kwa ajili ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa ajali mbaya ya kwanza kuwahi kutokea katika Kijiji hicho. Ajali hiyo ya Boti inayodaiwa kusababishwa na hali mbaya ya hewa katika ziwa hilo ilipelekea vifo vya watoto 11 na kinamama wawili. Mtoto mmoja na mama mmoja kati yao ni raia wa nchi jirani ya Zambia na tayari walishapelekwa nchini kwao kwa ajili ya taratibu za maziko. Abiria walookoelewa na kunusurika katika ajali hiyo ni 15 wakiwepo wakinamama 13 na watoto wawili, dereva wa boti hiyo mpaka msafara wa Mkuu wa Wilaya unaondoka kijijini hapo hakufahamika alipo. Abiria hao walikuwa wanatoka katika kijiji cha jirani cha Kapele kufata Zahanati kwa ajili ya chanjo, wakiwa njiani ndio wakapatwa na msiba huo. 
 
Muongozaji Mkuu wa Blogu ya Rukwareview Hamza Temba hakuwa nyuma kuhakikisha tukio hili zima linaruka hewani, hapo life jacket na kipenga mfukoni chochote kinaweza kutokea; Usalama Kwanza. "...tunashukuru Mungu tulienda salama na kurudi salama..."
 
Kijiji cha Kipwa kinavyoonekana kutokea ziwani (Tanganyika). Mpasuko wa milima unaoonekana ni kilele cha bonde na mto Kalambo  (Kalambo Falls).
 
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akimpa pole Ndugu Hassan Abdul ambaye ni mmoja wa wafiwa katika ajali hiyo mbaya ya boti ilyoua watoto 11 na kinamama wawili. Ofisi ya Wilaya ya Kalambo kwa kushirikiana na Chama Tawala (CCM) ilitoa ubani wa Tsh. 90,000/= kwa kila kaya iliyopatwa na msiba huo.
 

 Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akiwa amemshikilia mtoto Prisila Skapite (7) aliyefanikiwa kujiokoa katika ajali hiyo kwa kuogelea na kipande cha ubao hadi nchi kavu, mdogo wake aliyemshikilia alifanikiwa kuokolewa pia katika ajali hiyo.  
 
 Mama Roza Zunda naye alifanikiwa kujiokoa na mtoto wake kwa kumshikilia kama inavyoonekana pichani huku akiwa ameshikilia gunia la sabuni lililomsaidia kuogelea hadi nchi kavu na kuookolewa na waokoaji kutoka kijiji cha Kipwa baada ya kuishiwa nguvu. 
 
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea na wananchi wa kijiji cha Kipwa kilichopo mwambao wa Ziwa Tanganyika na kuwapa rambirambi za Serikali ambapo pia aliahidi kurudi katika kijiji hicho kufanya mikutano ya hadhara. Aliahidi kuwa Serikali itasaidia kujenga kituo cha afya katika kijiji hicho pamoja na kufuatilia ujenzi wa barabara itakayosaidia kuunganisha kijiji hicho na maeneo mengine ya Mkoa kutokana na ukweli kwamba kwa sasa kijiji hicho kinafikika kwa njia ya maji peke yake  kwa kutumia Boti.
 
 Afsa Mkuu wa SUMATRA Mkoa wa Rukwa (kulia) akiwa na DSO Wilaya ya Kalambo wakirudi kutoka katika Kijiji cha Kipwa kwa Boti mara baada ya kutembelea wahanga wa ajali hiyo mbaya ambayo haijawahi kutokea katika kijiji hicho.
  
Safari ya kurudi

Tuesday, September 24, 2013

"WALIOJENGA KATIKA MAENEO YASIYORUHUSIWA KISHERIA WABOMOE MARA MOJA" KAULI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizingumza katika kikao na wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wa hoteli katika Manispaa ya Sumbawanga tarehe 23 Septemba 2013 katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Pamoja na mambo mengine alipiga marufuku uchafuzi wa mazingira na kwamba watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupigwa faini. Kwa wale waliojenga katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria kama karibu na vyanzo vya maji amewataka kubomoa mara moja kwa mujibu wa sheria kabla hawajabomolewa kwa nguvu. Katikati ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta.
 
Sehemu ya Wafanyabiashara wakifuatilia moja ya mada katika kikao hicho.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisisitiza jambo katika kikao hicho. Aliwataka wafanyabiashara katika Manispaa ya Sumbawanga kuzingatia usafi katika maeneo yao ya biashara pamoja na kuacha tabia ya kutiririsha maji machafu katika mitaro ya maji taka na sehemu nyingine za mji ili kuweka Manispaa hiyo katika hali nzuri ya usafi.
 
Sehemu ya wafanyabiashara waliohudhuria katika kikao hicho.
 
Ndugu Dattoo ambaye ni Mfanyabiashara  wa Hoteli Mkoani Rukwa akitoa maoni yake katika kikao hicho ambapo alishauri ubora wa maji katika Mji wa Sumbawanga uboreshwe na vilevile wafanyakazi katika nyumba za kulala wageni waelimishwe juu hatari ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi pamoja na umuhimu wa kupima kujua afya zao. Hata hivyo kuna miradi mikubwa ya maji inaendelea kujegwa Mkoani Rukwa na Serikali na wadau wa maendeleo ambayo ikikamilika tatizo la maji litakuwa limekwisha katika Manispaa ya Sumbawanga.

Monday, September 23, 2013

MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA AFUNGUA KAMBI YA VIJANA WA CCM HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akishiriki kwa vitendo kufyatua matofali na vijana wa CCM walioweka kambi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga katika Mji mdogo wa laela tarehe 22 Septemba 2013. Lengo kuu la kambi hiyo ni kuwajenga vijana katika itikadi na sera za Chama cha Mapinduzi, Ukakamau na Uzalendo kwa chama na nchi yao kwa ujumla. Katika kambi hiyo wanajishughulisha pia na kazi za kijamii kama kufyatua matofali zaidi ya 6,000 yatakayosaidia katika kujenga kituo cha afya Laela. Katika kuwapa nguvu kuendeleza kambi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa mchango wa laki mbili taslim.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Mbunge viti maalum CCM Mkoa wa Ruvuma akiwahamsisha vijana hao kukipenda chama chao kwa kuweka uzalendo mbele katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Chama hicho katika mji mdogo wa Laela tarehe 22 Septemba 2013. Kutoka kushoto ni Matin Matete Mjumbe wa baraza kuu CCM taifa, C. Bakuli Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Rukwa, Injinia Manyanya RC Rukwa, Godwin Mzurikwao Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Rukwa, Ali Mgaya Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini na Persin Kalikule Mhamasishaji UVCCM Mkoa wa Rukwa.
 
Sehemu ya vijana hao waliotoka katika maeneo tofauti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakionekana kuhamasika vya kutosha katika kambi hiyo iliyopo katika mji mdgo wa Laela.
 
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa (UVCCM) Godwin Mzurikwao  akielezea mipango mbalimbali ya umoja huo ikiwemo uhamasishaji na upandaji miti ya mbao kwa ajili ya kuwainua vijana kiuchumi Mkoani Rukwa. Katikati akisikiliza kwa umakini ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi ndugu Ali Mgaya Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini miti na viriba vya kupandia miti ya mbao ambayo ni sehemu ya mpango wa UVCCM Mkoa wa Rukwa kuwawezesha na kuwahamasisha vijana katika zoezi la upandaji miti wa kibiashara.

Saturday, September 21, 2013

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMIVU YA CHUO KIKUU CHA GUELPH JIMBONI ONTARIO, CANADA

t7
Sehemu ya umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013

 t9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa Shahada ya Uzamivu na Provost na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario, Dkt Maureen Mancuso , Ijumaa Septemba 20, 2013
 
t10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa katika Chuo Kikuu Guelph baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013.
 
 t11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Chuo Kikuu Guelph baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013
 
 t12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013
 
 t13
Umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013
 
 t15
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Wakuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013
 
t16
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013
 
t17
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013
PICHA NA IKULU

……………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Ijumaa, Septemba 20, 2013, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) na Chuo Kikuu cha Guelph katika jimbo la Ontario nchini Canada kwa kutambua mchango na uongozi wake katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.
  
Viongozi wa Chuo hicho wanasema kuwa wamefanya uamuzi wa kumtunuku Rais Kikwete kutokana na jitihada zake za kukabiliana na changamoto zinazokabili kilimo, jitihada zake za kuleta usalama wa chakula na pia majaribio makubwa ya kuongeza matumizi ya technolojia katika kilimo cha Tanzania na Afrika.
 
Rais Kikwete ambaye amewasili Canada usiku wa Alhamisi, Septemba 19, 2013 akitokea Washington, D.C., Marekani ambako alikuwa kwa siku mbili akitokea Jimbo la California amekuwa Mtanzania wa kwanza kutunukiwa shahada ya juu kabisa katika historia ya Chuo hicho.
 
Chuo cha Guelph ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa zaidi katika Canada na duniani katika Nyanja za kilimo na kilianzishwa rasmi kama Chuo cha Kilimo cha Jimbo la Ontario Mei Mosi, mwaka 1874.
 
Chuo hicho ambacho kimejipatia umaarufu kutokana na ubora wa shughuli zake za utafiti kimekuwa katika mstari wa mbele kutafuta majawabu ya changamoto zinazoikabili dunia katika masuala ya kilimo, raslimali za maji, matatizo makubwa ya magonjwa ya mimea, matatizo ya ukuaji haraka wa miji duniani na changamoto za biashara za kimataifa.
 
Katika miaka ya karibuni kufuatia tishio kubwa kimataifa la ongezeko la bei za vyakula duniani na hasa katika nchi masikini, mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la uchafuzi wa hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama duniani, kazi ya Chuo hicho imeongezeka sana.
Chuo hicho kimeichagua Tanzania kama nchi ya kufanya nayo kazi katika Afrika kukabiliana na changamoto hizo na kimemtambua Rais Kikwete kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo katika miaka yote ya uongozi wake na mipango yake ya kuboresha kilimo katika Tanzania kama ASDP, Kilimo Kwanza na SAGCOT ambayo yote inasifiwa sana kimataifa.
 
Chuo hicho kina mahusiano ya karibu na Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na UDOM – Dodoma. Kati ya mwaka jana na mwaka huu, Chuo hicho kimetiliana saini Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mara nne kati ya Januari, mwaka jana, 2012 na Juni, mwaka huu, 2013, uongozi wa Chuo hicho ukiongozwa na Rais na Makamu Mkuu wa Chuo, Dkt. Alastair Summerlee na Makamu wa Rais wa Utafiti Dkt. Kevin Hall umetembelea Tanzania na kukutana na viongozi wa Serikali pamoja na wale wa Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam na Sokoine cha Mzumbe, Morogoro.
 
Mbali na ujumbe ambao unaongozana na Rais Kikwete, sherehe za kutunukiwa kwa Kiongozi Mkuu huyo wa Tanzania pia zimehudhuriwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Jumuia ya Watanzania wanaoishi Canada pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.
 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
20 Septemba, 2013

Friday, September 20, 2013

FHI 360 WAISHUKURU OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA KWA MSAADA WA OFISI NA USHIRIKIANO WA KARIBU WALIOUPATA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiongea na Afisa Mwandamizi mradi wa FHI 360 Road II Bi Florence Lema na Mratibu wa Mradi eneo la Sumbawanga Ndugu Nsajigwa Richard walipofika ofisini kwake leo kushukuru kwa msaada wa ofisi waliopewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambayo waliitumia kwa muda wa miaka mitatu. 
 
Afisa Mwandamizi mradi wa FHI 360 Road II Bi Florence Lema akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima barua ya shukurani kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kuwasaidia Ofisi waliyoitumia kwa mda wa miaka mitatu katika kipindi chote cha mradi ambao ambao hivi sasa umekamilika.
 

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akionyesha barua hiyo mara baada ya kukabidhiwa ofisi iliyokuwa ikitumika na mradi wa FHI 360 Road II Mkoani Rukwa. Afisa Mwandamizi wa mradi huo Bi. Florence Lema ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano Mkubwa ilionao katika kusaidia na kujumuika pamoja na sekta binafsi na mashirika ya kijamii ya kitaifa na kimataifa.
 
 
Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na wawakilishi kutoka FHI 360 Ofisi kwake mapema hii leo.