Wednesday, September 11, 2013

MIRADI HII MIKUBWA YA MAJI IKIKAMILIKA TATIZO LA MAJI KATIKA MJI WA SUMBAWANGA KUWA HISTORIA

Hatua za awali za mradi wa kujenga Tanki la maji lenye ujazo wa lita Milioni moja (m3 1,000) katika eneo Kilimani katika Manispaa ya Sumbawanga.
 
Kupitia mradi wa Maendeleo ya  sekta ya maji (Water Sector DevelopmentProgramme) miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Tanzania na wafadhili mbalimbali wakiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, Umoja wa Ulaya na wengineo inaendelea kujengwa Mkoani Rukwa. 

 
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bwana Samson Mashalla pamoja Mhandisi wa Maji Skretarieti ya Mkoa huo Emmy George wakiongea na wafanyakazi wa kampuni ya Technofab-Garmon JV wa New Delhi India ambao ndio Mkandarasi wa mradi huo wa ujenzi wa matanki 6 ya kuhifadhia maji lita milioni 7, mabwawa ya kumwagia maji taka, nyumba tatu za watumishi, Kulaza bomba kuu km 16 na za kusamabaza maji km 60. Kununua magari 3 ya majitaka na 2 ya kutembelea. Kununua na kufunga Booster pump 2 na Kupanua mtambo wa kusafisha maji kwa kujenga Rapid sand filters. 

Hatua za awali za mradi wa kujenga Tanki la maji lenye ujazo wa lita Milioni mbili (m32,000) katika eneo Majengo katika Manispaa ya Sumbawanga.Hatua za awali za mradi wa kujenga Tanki la maji lenye ujazo wa lita Milioni moja (m3 1,000) katika eneo la Katanda katika Manispaa ya Sumbawanga.
Ujenzi ukiwa unaendelea katika kituo hicho cha Katandala. Hapa zinajengwa ofisi, tanki la maji pamoja na mitambo ya kusambazia maji katika Manispaa ya Sumbawanga. 

Mkurugenzi wa SUWASA Ndugu Shirima akitoa maelezo kwa wajumbe wa msafara ulioongozwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ndugu Samson Mashalla walipotembelea sehemu mbalimbali za ujenzi wa miradi ya maji ikiwemo huu wa kujenga mabwawa ya kumwagia maji taka katika Manispaa ya Sumbawanga. 
Uchimbaji wa visima vya maji ukiendelea katika maeneo tofauti Mkoani Rukwa. (Sumbawanga Mjini). Mkandarasi wa mradi huu ni Jandu Plumbers na Metito JV wa Arusha ambao wanachimba na kujenga visima 12 vyenye wastani wa kina cha mita 150 vyenye uwezo wa kuzalisha jumla ya mita za ujazo 13,040 kwa siku.

Ujenzi wa tanki la maji na mashine za kusukuma maji katika Manispaa ya Sumbawanga, mradi huu wa "Lwiche Water Fill" uliopo katika kijiji cha Kankwale katika Manispaa ya Sumbawanga. Mkandarasi anaejenga mradi huu uliofadhiliwa na benki ya dunia anaitwa Herkens Builders ya Dar es Salaam.
 
Mashine za kusukuma maji katika mradi wa "Lwiche Water Fill" uliopo katika kijiji cha Kankwale katika Manispaa ya Sumbawanga. Mkandarasi anaejenga mradi huu uliofadhiliwa na benki ya dunia anaitwa Herkens Builders ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment