Tuesday, September 17, 2013

MKEMIA MKUU WA SERIKALI AONANA NA MKUU WA MKOA WA RUKWA, AOMBA KILA MKOA UTOE TAMKO LA KUPAMBANA NA MATUMIZI MABAYA YA TINDIKALI NCHINI

 
Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya zawadi ya kitini na CD vya somo la Kemia kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Mkoani Rukwa katika hafla fupi alipoongea na waalim wakuu wa shule za Sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 17 Septemba 2013 katika ukumbi wa RDC mkoani Rukwa. Alisema kuwa kwa sasa kuna umuhimu mkubwa wa wanafunzi kuhamasishwa kusoma masomo sayansi na kuelimishwa zaidi juu ya matumizi sahihi ya tindikali tofauti na hivi sasa inavyotumika kama silaha ya kuwadhuru watu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akionyesha CD na kitini alichokabidhiwa na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajii ya kuvisambaza katika shule za Sekondari Mkoani Rukwa. Mkemia Mkuu wa Serikali alisema hiyo ni sehamu ya Mpango wa Ofisi yake na Serikali kuboresha somo la Kemia hapa nchini. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Chima.

 Picha ya pamoja kati ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa na waalimu wakuu wa Shule za Sekondari Mkoani Rukwa.
 
Profesa akutana na Mwalimu wake: Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na mwalimu wake Ndugu John Maufi aliowahi kumfundisha katika shule ya Sekondari Kantalamba Mkoani Rukwa. Mkemia Mkuu wa Serikali aliwahi kuwa mwanafunzi bora wa somo la sayansi hapa nchini mnamo mwaka 1987. Kwasasa Mwalim Maufi ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya St. Theresia ya Mkoani Rukwa.  
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkemia Mkuu wa Serikali alipomtembelea ofisini kwake mapema leo. Mkuu huyo wa Mkoa alikiri kuwa jamii kwa sasa ina umuhimu mkubwa wa kujifunza juu ya matumizi na uhifadhi wa tindikali kuepusha madhara yanayojiotokeza ya kutumika ndivyo sivyo, alisema kuwa jamii ina wajibu wa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha inawafichua wahalifu wanaotumia tindikali kuwadhuru watu wengine.

No comments:

Post a Comment