Tuesday, September 24, 2013

"WALIOJENGA KATIKA MAENEO YASIYORUHUSIWA KISHERIA WABOMOE MARA MOJA" KAULI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizingumza katika kikao na wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wa hoteli katika Manispaa ya Sumbawanga tarehe 23 Septemba 2013 katika ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Pamoja na mambo mengine alipiga marufuku uchafuzi wa mazingira na kwamba watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupigwa faini. Kwa wale waliojenga katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria kama karibu na vyanzo vya maji amewataka kubomoa mara moja kwa mujibu wa sheria kabla hawajabomolewa kwa nguvu. Katikati ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta.
 
Sehemu ya Wafanyabiashara wakifuatilia moja ya mada katika kikao hicho.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akisisitiza jambo katika kikao hicho. Aliwataka wafanyabiashara katika Manispaa ya Sumbawanga kuzingatia usafi katika maeneo yao ya biashara pamoja na kuacha tabia ya kutiririsha maji machafu katika mitaro ya maji taka na sehemu nyingine za mji ili kuweka Manispaa hiyo katika hali nzuri ya usafi.
 
Sehemu ya wafanyabiashara waliohudhuria katika kikao hicho.
 
Ndugu Dattoo ambaye ni Mfanyabiashara  wa Hoteli Mkoani Rukwa akitoa maoni yake katika kikao hicho ambapo alishauri ubora wa maji katika Mji wa Sumbawanga uboreshwe na vilevile wafanyakazi katika nyumba za kulala wageni waelimishwe juu hatari ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Ukimwi pamoja na umuhimu wa kupima kujua afya zao. Hata hivyo kuna miradi mikubwa ya maji inaendelea kujegwa Mkoani Rukwa na Serikali na wadau wa maendeleo ambayo ikikamilika tatizo la maji litakuwa limekwisha katika Manispaa ya Sumbawanga.

No comments:

Post a Comment