Saturday, January 25, 2014

SITASITA KUWAONDOA WATUMISHI / WAKUU WA IDARA WANAOWACHONGANISHA MADIWANI NA MKURUGENZI WAO - ASEMA INJINIA MANYANYA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kilichofanyika jana tarehe 25 Januari 2014 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo Sumbawanga Mjini. 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza katika kikao hicho ambapo alitilia mkazo juu kuboresha elimu na ufaulu katika halmashauri hiyo ambayo haijafanya vizuri katika siku za karibuni. Alisisitiza pia umuhimu wa upandaji miti hususani katika msimu huu wa masika.
Mbunge wa Jimbo la Kwela (CCM) Ignas Malocha akishukuru ujio wa Mkuu huyo wa Mkoa katika kikao hicho na maelekezo aliyoyatoa ambayo alisema ni muongozo mzuri na wa kuzingatiwa katika maendeleo ya halmshauri hiyo.
Mkuu huyo wa Mkoa akizungumza na wajumbe wa kikao hicho kushoto wakiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na kulia wakiwa ni wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.
Madiwani wa halmashauiri ya wailaya ya Sumbwanga.
Wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Sumbwanga.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Madiwani na Viongozi wa Chama tawala (CCM) walioalikwa katika kikao hicho.

........................................................

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya amewaonya watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakiwemo wakuu wa idara wenye tabia ya kuwachonganisha madiwani na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Adam Misana, "watumishi mnaofanya mchezo huo nitawaondoeni" Alisema Manyanya. 

Manyanya aliyasema hayo jana katika kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga alipotembelea kutoa salam zake za mwaka mpya kwenye baraza hilo. Alisema kuwa tangu Mkurugenzi huyo ateuliwe kuiongoza Halmashauri hiyo amekuwa akifanya vizuri katika udhibiti wa mapato jambo ambalo limekuwa kero kubwa wakuu wa idara na watumishi wa ofisi hiyo.

Alieleza kuwa Mkurugenzi aliyekuwepo kabla ya Misana alikua akikaimisha ofisi mara kwa mara kwa watu tofauti jambo ambalo lilizorotesha utendaji na kupelekea mambo kufanyika kienyeji na kwa mazoea bila kujali matumizi sahihi ya mapato ya Halmashauri. Ujio wa Mkurugenzi huyu mpya umerekebisha hali hiyo kwa kiwango kikubwa hususani katika matumizi ya fedha za halmashauri, aliongeza Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika salam zake alilieleza baraza hilo kuwa mpaka sasa toka ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ameshatembelea kata 51 sawa na asilimia 80% ya kata zote Mkoani Rukwa. Alisema baadhi ya kata hizo ameshazitembelea zaidi ya mara tano kutokana na umuhimu na matukio yaliyojitokeza.

Aliwata madiwani, viongozi wa chama na halmashauri pamoja watumishi kwa ujumla kutoa uongozi uliotukuka katika maeneo yao kwa kushirikiana katika kutoa huduma bora kwa wanachi na kuwafikia mara kwa mara pale inapowezekana na kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Katika hali nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alishangazwa kwa Wilaya ya Sumbwanga kutokuwa na Hospitali yake ya Wilaya na badala yake kutegemea huduma katika Hospitali  Kuu ya Mkoa. Alisema mwaka huu 2014 ni mwaka wa afya na kwamba Halmashauri za Wilaya ya Sumbwanga zijipange kuhakikisha zinakuwa na hospitali yao ya Wilaya ili kuweza  kutoa nafasi kwa hospitali kuu ya Mkoa kuhudumia wagonjwa wa rufaa kuliko ilivyo hivi sasa ambapo ambapo inabebeshwa mzigo mkubwa na Wilaya hiyo.

Katika salam zake Injinia Manyanya aliwashauri madiwani na viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kujipanga kuhakikisha wanahamia katika Mji mdogo wa Laela uliopo takribani kilomita 100 kutoka mjini Sumbawanga. Alisema zipo faida kubwa za kufanya hivyo ikiwemo ya halmasahuri kuwa na mji wake watakaouendeleza kisasa na kujiwekea mikakati mbalimbali ya kimaendeleo. Aliongeza pia kuwa itakuwa fursa ya kuwasogezea wananchi huduma.

 Akielezea kuhusu jengo kubwa la kisasa la Halmashauri hiyo linaloendelea kujengwa mjini Sumabwanga alisema linaweza kutumika kama kitega uchumi cha Halmashauri ambapo litawapatia fedha nyingi za kujiendesha na kwamba wataomba fedha nyingine TAMISEMI ya kujenga ofisi kubwa kama hiyo Laela kwa lengo la kuwasogezea wananchi huduma.

Akizungumzia kilimo na ufugaji aliwataka viongozi wa halmashauri wakishirikiana na madiwani kuhakikisha wanajiwekea utaratibu maalumu wa maeneo ya wakulima na wafugaji na kuhakikisha kunakuwepo na idadi maalum ya mifugo inayotakiwa kufugwa katika maeneo yaliyotengwa na kuwekewa alama maalum za utambuzi.

Kwa upande wa ONYARU - Ondoa Nyasi Rukwa alisema kuwa mpango huu umekuwa na mafanikio makubwa kwani maeneo mengi wananchi wamehamasika kwa kuondoa nyasi na kuezeka kwa bati nyumba zao. Aliwataka viongozi na wasimamizi wa halmashauri kuendelea na uhamasihaji huo kuhakikisha nyumba za nyasi zinauhama Mkoa wa Rukwa.  

Thursday, January 23, 2014

BARAZA LA HALMASHAURI LA WILAYA YA KALAMBO LAPITISHA BAJETI MPYA YA MWAKA WA FEDHA 2014/2015 YA TSH. BILIONI 27.4

Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akichangia
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a akichangia mawazo yake katika kikao hicho.
Sehem ya Waheshimiwa madiwani wafuatilia
Sehemu ya Waheshimiwa madiwani wafuatilia mambo mbalimbali katika kikao hicho
Sehemu ya wakuu wa idara wakifuatilia kikao hicho

…………………………………………………………………………………

NA RAMADHANI JUMA OFISI YA MKURUGENZI KALAMBO
Baraza madiwani la Halmashauri ya wilaya Kalambo Mkoa wa Rukwa limepitisha bajeti ya mwaka 2014/2015 itakayoanza kutekelezwa mwezi Julai mwaka huu.

Katika kikao chake cha jana kilichofanyika mjini Matai wilayani humo, baraza hilo lilijadili na kupitisha shilingi bilioni 27,445,547,650 kuwa bajeti ya halmashauri hiyo katika mwaka ujao wa fedha.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Philbert Ngaponda, fedha hizo zitatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ambayo ni shilingi 1,023,611,000 na ruzuku ya serikali kuu kwa ajili ya mishahara shilingi 13,555,354,700.

Chanzo kingine ni ruzuku kwa ajili  ya miradi ya maendeleo ambayo ni shilingi 11,224,181,450 na ruzuku kutoka serikali kuu kwa ajili ya matumizi mengine ya ofisi ambayo ni shilingi1,642,400,504.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa, bajeti hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo sera za serikali, ukomo wa bajeti, pamoja vipaumbele vya kitaifa.

Wednesday, January 22, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA WATUMISHI WA HOSPITALI KUU YA MKOA KUSKILIZA KERO ZAO KWA AJILI YA KUZIPATIA UFUMBUZI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye kikao na watumishi wa idara ya afya wa hospitali kuu ya Mkoa iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga. Alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero, malalamiko pamoja na ushauri kwa ajili ya kuboresha huduma na utendaji katika hospitali hiyo. Kero mbalimbali zilitolewa ikiwepo upandishwaji wa vyeo kuchukua mda mrefu, kubadilishiwa muundo wa vyeo na kusababisha kupungua kwa mishara kimakosa, uhaba wa vitendea kazi pamoja na madaktari bingwa wa upasuaji ambapo kwa sasa hamna hata mmoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya kusikiliza kero mbalimbali aliagiza uongozi wa hospitali hiyo kutatua kero zilizo chini ya uwezo wao na zile nyingine kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa kuzishirikisha mamlaka husika. Kushoto ni Mganga Mkuu hospitali ya Mkoa Rukwa Dkt. William Gurisha. Kero nyingi zimeonekana kuibuka kutokana na uhaba wa fedha za OC kutofika kwa wakati na kwa kiwango kilichopangwa. Hata hivyo hospitali hiyo imeonekana kujipanga kutumia vyanzo vya mapato ya ndani kutatua baadhi ya kero hizo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla akifafanua baadhi ya mambo ya kiutawala katika kikao hicho. 
Wajumbe katika kikao hicho.
Mmoja ya wahudumu wa afya akitoa kero yake.

Tuesday, January 21, 2014

ALIYEKUA KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA SASA MKOA WA TANGA NDUGU SALUM MOHAMMED CHIMA AAGA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA TAYARI KWENDA KURIPOTI TANGA

Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Tanga aliyehamishwa kutoka Mkoa wa Rukwa Ndugu Salum Mohammed Chima akizungumza katika hafla fupi ya kuagana na uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya (kulia) leo baada ya mabadiliko ya hivi karibuni ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete ambapo ameteua Makatibu Tawala wapya watano na kuhamisha wengine akiwepo Ndugu Salum Chima. Katika salamu zake za kuaga ameomba viongozi wote wa Mkoa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha wanasimamia kikamilifu na kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa ya Serikali na wahisani mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa salam zake za maagano ambapo alisikitika kwa uhamisho wa kiongozi huyo ambaye kwake alikua kiungo muhimu na msaada mkubwa katika mambo ya kiutendaji. Aidha alisisitiza juu ya kuchapa kazi na ushirikiano baina ya viongozi wa Mkoa na wananchi katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akitoa neno kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Rukwa, alisema kuwa kwa Ndugu Chima kuhamishiwa Mkoa wa Tanga ambao ni Jiji akitokea Mkoa mdogo wa Rukwa ni "promotion" na anastahiki pongezi kwani uwezo wake wa kuchapa kazi ndo umemfikisha hapo alipo. Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa sifa kubwa ya Ndugu Chima ni uwezo wake mkubwa wa kutoa maamuzi sahihi na ya haraka kwa wakati sifa ambayo ni muhimu kwa viongozi wa sasa katika maendeleo ya taifa letu.
Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Ndugu Samson Mashalla (kulia) akiongea kwa niaba ya watumishi wote wa Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa. Alieleza kushtushwa na uhamisho huo uliokuwa wa ghafla ambapo kwa watumishi umekuwa ni kusikitisha kutokana na ukaribu, upole na upendo aliokuwa nao Ndugu Chima. Ndugu Chima aliwapenda watumishi wote wa ngazi za juu hadi za chini bila ubaguzi wa aina yeyote.
Baadhi ya viongozi na watumishi walihudhuria katika hafla hiyo fupi ya maagano. WATUMISHI WOTE NA VIONGOZI WA SERIKALI YA MKOA WA RUKWA WANAMTAKIA NDUGU CHIMA KILA LA HERI KATIKA KITUO CHAKE KIPYA CHA KAZI AMBACHO NI MKOA WA TANGA. Tunaamini kuwa Tanga imepata kiongozi thabiti mwenye uwezo mkubwa wa kuongoza katika kutoa maamuzi sahihi na ya haraka kwa muda muafaka, "tunaomba apewe ushirikiano atafanya". Kwa upande wake Katibu Tawala Mteule wa Mkoa wa Rukwa kwa sasa ndugu Symthies E.Pangisa aliyekuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara anakaribishwa kwa dhati Mkoani Rukwa na ameahidiwa ushirikiano katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. 

Monday, January 20, 2014

Majina ya Uhamisho na Uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri Uliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete Leo Hii,Mawaziri Wapya ni Pamoja na Dr Asha Rose Migiro,Juma Nkamia,Mwigulu Nchemba,Jenista Mhagama,Godfrey Zambi

  Naibu Wizara Mpya wa Fedha (Sera)Mwigulu Nchemba
 Naibu Waziri Mpya wa  kilimo na Chakula-Godfrey Zambi
 Waziri Mpya wa Katiba na Sheria Dr Asha Rose Migiro
Naibu Waziri Mpya wa wizara ya Jinsia na watoto Pindi Chana
 Naibu Waziri Mpya wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Jenista Muhagama.
   Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue.akitangaza baraza la mwaziri leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Kwa Makini Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue(hayupo pichani)akitangaza baraza la mwaziri Ikulu Jijini Dar es Salaam
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewahamisha na kuwateua baadhi ya Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:-

1.0 OFISI YA RAIS

Hakuna mabadiliko.

2.0 OFISI YA MAKAMU WA RAIS

2.1 Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko

2.2 Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)
Waziri wa Nchi (Mazingira).

2.3 Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)
Naibu Waziri 

3.0 OFISI YA WAZIRI MKUU

Hakuna mabadiliko

4.0 WIZARA

4.1 WIZARA YA FEDHA
4.1.1 Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)
Waziri wa Fedha
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb) 
Naibu Waziri wa Fedha
4.1.2 Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha


4.2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Hakuna mabadiliko


4.3 WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

4.3.1 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
Waziri wa Katiba na Sheria

4.3.2 Naibu Waziri – Hakuna mabadiliko

4.4 WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Hakuna mabadiliko

4.5 WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

4.5.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

4.5.2 Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

4.6 WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA

Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa


4.7 WIZARA YA UJENZI

Hakuna mabadiliko

4.8 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

4.8.1 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
Waziri wa Mambo ya Ndani

4.8.2 Naibu Waziri – Hakuna Mabadiliko


4.9 WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

4.9.1 Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

4.9.2 Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

4.10 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

4.10.1 Waziri: Hakuna mabadiliko

4.10.2 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

14.11 WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

14.11.1 Waziri: Hakuna mabadiliko

14. 11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

14.12 WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

14.12.1 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

14.12.2 Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

14.13 WIZARA YA KAZI NA AJIRA

Hakuna mabadiliko

14.14 WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Hakuna mabadiliko
14.15 WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

14.15.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

14.15.2 Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

14.16 WIZARA YA MAJI

14.16.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

14.16.2 Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji

14.17 WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA

14.17.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

14.17.2 Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

4.18 WIZARA YA UCHUKUZI

Hakuna mabadiliko

4.19 WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

4.19.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

4.19.2 Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

4.20 WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii

4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

4.21 WIZARA YA NISHATI NA MADINI

4.21.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

4.21.2 Naibu Waziri (Madini) – Hakuna mabadiliko

4.21.3 Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)

Naibu Waziri (Nishati)

Balozi Ombeni Y. Sefue
KATIBU MKUU KIONGOZI

Ikulu
DAR ES SALAAM

19 Januari, 2014

Sunday, January 19, 2014

RAIS KIKWETE ATEUA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA WATANO NA KUHAMISHA WENGINE NA WAKURUGENZI WA MAJIJI

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
 Rais Mheshimiwa Dkt Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa makatibu tawala wa mikoa mitano na kuwahamisha makatibu tawala wengine na wakurugenzi wa majiji.

Makatibu tawala wapya ni ndugu Wamoja A.Dickolangwa anayeenda mkowa wa Iringa ambako alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa,ndugu Abdallah D.Chikota anayeenda Lindi kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Newala,ndugu Symthies E.Pangisa anayeenda mkoa wa Rukwa kabla alikuwa kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mtwara,ndugu Alfred C.Luanda aliyeteuliwa kuwa katibu tawala mkoa wa Mtwara kabla alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Tabora,ndugu Jackson L.Saitabau anakwenda mkoa wa Njombe kabla alikuwa katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Arusha.

Waliohamishwa ni Beatha Swai kutoka katibu tawala mkoa wa Pwani kwenda ofisi ya waziri mkuu,TAMISEMI,ndugu Sipora J.Liana,kutoka mkurugenzi wa jiji la Arusha kwenda ofisi ya waziri mkuu,TAMISEMI,ndugu Benedict ole Kuyan kutoka katibu tawala mkoa wa Tanga kwenda katibu tawala mkoa wa Mara,ndugu Salum M.Chima kutoka katibu tawala Rukwa kwenda Tanga na Ndugu Mgeni Baruani kutoka katibu tawala mkoa wa Njombe kwenda katibu tawala mkoa wa Pwani.

Wengine ni Ndugu Juma R. Idd kutoka mkurugenzi wa jiji la Mbeya na kuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha,Eng.Omar Chambo aliyekuwa katibu mkuu wizara ya uchukuzi amehamishiwa mkoa wa Manyara kama katibu tawala wa mkoa,Dkt John Ndunguru aliyekuwa naibu katibu mkuu wa wizara ya ujenzi anahamishiwa mkoa wa Kigoma kama katibu tawala wa mkoa huo.

Imetolewa na:
Kurugenzi Ya Mawasiliano Ya Rais,
DAR ES SALAAM
18 January 2013

Friday, January 17, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA TIMU MAALUUM YA KUHAKIKI MAENEO MAPYA YA UTAWALA KUTOKA TAMISEMI, AISHAURI MAMLAKA HUSIKA KUANGALIA UPYA VIGEZO VINAVYOTUMIKA KUGAWA MAENEO MAPYA YA UTAWALA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na timu maalum inayohakiki maeneo mapya ya utawala kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Pichani kulia na timu yake ya Mkoa iliyokuwa ikiratibu maeneo hayo ofisini kwake leo tarehe 17 Januari 2014. Timu hiyo kutoka TAMISEMI inaongozwa na Mwanasheria wa TAMISEMI Ndugu Eustard Ngatale (watatu kulia).

 Katika kikao hicho kifupi Mkuu huyo wa Mkoa ameiomba mamlaka husika kupitia timu hiyo kuangalia upya vigezo vinavyotumika katika kugawa maeneo mapya ya utawala na upandishaji wa madaraja kutoka kijiji, kata, Tarafa, Halmashauri, Miji na Manispaa. 

Alisema kuwa kuna maeneo mengine ambayo yakiangaliwa kwa kigezo kimoja cha wingi wa watu bila kuangalia umbali wa huduma na giografia ya eneo husika unakuta wananchi wanakosa huduma zao za msingi na kupata tabu kubwa katika kuzipata.

 Alitolea mfano vijiji vikubwa vya mwambao ambavyo kupata huduma katika kata zao ni lazma wavuke upande mmoja wa Ziwa kwenda upande mwingine jambo ambalo ni hatarishi kama ilivyotokea kwa wananchi wa Kijiji cha Kipwa Mwambao mwa Ziwa Tanganyika ambao hivi karibuni walipoteza watu 15 katika ajali ya boti walipokwenda kupata huduma ya afya. Wengi ya waliofariki katika ajali hiyo mbaya walikuwa ni watoto chini ya umri wa miaka 5.  
Kikao kikiwa kinaendelea ambapo kwa upande wake Mwanasheria wa TAMISEMI Ndugu Eustard Ngatale alisema kuwa kubariki na kuhalalisha uanzishwaji wa maeneo mapya ya Utawala vipo vitu mbalimbali vya kuzingatia ambavyo ni pamoja na kuwepo kwa makubaliano ya wananchi na viongozi wa maeneo husika kupitia mihutasari ya vikao maalumu vya kisheria vya WDC, Halmashauri, DCC na RCC katika ngazi ya Mkoa.

Wednesday, January 15, 2014

RAIS KIKWETE AMUAPISHA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA NA KAMISHNA WA TUME YA USULUHISHI

D92A7710Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewaapisha Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Kamishna wa Tume ya usuluhishi na Uamuzi.Walioapishwa leo katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam ni Dkt.Aziz Ponary Mlima anayekuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia na Bwana Jafari Omari anayekuwa Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.
Pichani D92A7748Kamishna wa Tume ya usuluhishi na uamuzi Bwana Jafari Omari akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo
asubuhi. D92A7780
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wateule aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bwana Jafari Omari na kulia ni Balozi mpya wa Tanzania nchini Malaysia Dkt.Aziz Ponary Mlima (picha na Freddy Maro).

Tuesday, January 14, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA AVAMIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WIILAYA YA NKASI, AWATAKA KUBORESHA MAKUSANYO YA MAPATO YA HALMASHAURI YAO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia baraza kuu la madiwani wa Wilaya ya Nkasi (Full Council) lililokua kwenye kikao cha kujadili na kupitisha bajeti ya fedha ya mwaka 2014/2015 na kupitisha sheria ndogondogo za halmashauri. Katika hotuba yake aliwataka madiwani na viongozi wa halmashauri na wilaya ya Nkasi kushirikiana kwa pamoja na kuweka pembeni itikadi zao katika kuunda vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia kwa kuwekeana mikakati maalum ya makusanyo kwa kila kijiji, kata, tarafa, halmashauri na Wilaya kwa ujumla. Alisema halmshauri hiyo haitaweza kuendelea kwa kuendelea kuwa tegemezi kutoka Serikali kuu na badala yake waongeze makusanyo ya ushuru na mapato yasaididie katika mipango ya kujiendeleza. Kikao hicho kilipitisha bajeti ya Tsh Bilioni 25.4.Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akizungumza katika kikao hicho ambapo alisisitiza juu ya kuboresha na kusimamia upatikanaji wa mapato ya halmashauri ambayo pamoja na mambo mengine yatasaidia katika kuboresha miundombinu ya barabara katika Wilaya hiyo ambayo imekua ndio kilio kikubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Albinus Mugonya.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika kikao hicho. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Peter Mizinga.
Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi waliohudhuria kikao hicho.Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.