Thursday, January 23, 2014

BARAZA LA HALMASHAURI LA WILAYA YA KALAMBO LAPITISHA BAJETI MPYA YA MWAKA WA FEDHA 2014/2015 YA TSH. BILIONI 27.4

Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a akichangia
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a akichangia mawazo yake katika kikao hicho.
Sehem ya Waheshimiwa madiwani wafuatilia
Sehemu ya Waheshimiwa madiwani wafuatilia mambo mbalimbali katika kikao hicho
Sehemu ya wakuu wa idara wakifuatilia kikao hicho

…………………………………………………………………………………

NA RAMADHANI JUMA OFISI YA MKURUGENZI KALAMBO
Baraza madiwani la Halmashauri ya wilaya Kalambo Mkoa wa Rukwa limepitisha bajeti ya mwaka 2014/2015 itakayoanza kutekelezwa mwezi Julai mwaka huu.

Katika kikao chake cha jana kilichofanyika mjini Matai wilayani humo, baraza hilo lilijadili na kupitisha shilingi bilioni 27,445,547,650 kuwa bajeti ya halmashauri hiyo katika mwaka ujao wa fedha.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Philbert Ngaponda, fedha hizo zitatokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ambayo ni shilingi 1,023,611,000 na ruzuku ya serikali kuu kwa ajili ya mishahara shilingi 13,555,354,700.

Chanzo kingine ni ruzuku kwa ajili  ya miradi ya maendeleo ambayo ni shilingi 11,224,181,450 na ruzuku kutoka serikali kuu kwa ajili ya matumizi mengine ya ofisi ambayo ni shilingi1,642,400,504.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa, bajeti hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia mambo mbalimbali ikiwemo sera za serikali, ukomo wa bajeti, pamoja vipaumbele vya kitaifa.

No comments:

Post a Comment