Friday, January 10, 2014

KAMATI MAALUM YA WANANCHI WA KIJIJI CHA SKAUNGU WANAOFATILIA MGOGORO KATI YAO NA MUWEKEZAJI EPHATA MINISTRY WAONANA NA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiiskiliza kwa makini kamati maalum ya wananchi wa Skaungu iliundwa kufuatilia maendeleo ya mgogoro unaowakabili wa shamba la Skaungu na muwekezaji Ephata Ministry. Kamati hiyo ilikuwa na kiu ya kujua hatma ya mgogoro huo ambao inadaiwa kuwa sehemu ya shamba alilouziwa muwekezaji huyo lipo ndani ya kijiji chao. Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi hao wawe watulivu kwani Serikali inachukua hatua ya kumaliza mgogoro huo. Alisema kuwa Kamati maalum ya bunge inayoshuulikia migororo ya ardhi itawasili Mkoani Rukwa tarehe 11 Januari 2014 kwa ajili ya kuonana na wananchi na kujionea uhalisia kwa ajili ya kulishauri Bunge na Serikali namna ya kumaliza mgogoro huo, aidha aliongeza kuwa wapimaji kutoka wizarani watawasili pia Mkoani hapa ambapo watashirikiana na wapimaji waliopo Mkoani Rukwa kwa ajili ya kupima maeneo ya mipaka iliyopo ya vijiji na shamba hilo ili hatua zaidi za kimaamuzi ziweze kuchukuliwa. Aliwataka wananchi wa vijiji vinavyozunguka shamba hilo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kamati hiyo ili iweze kufanya kazi iliyowaleta kirahisi.
Kamati hiyo iliyokuwa na wajumbe watano iliongozwa na Mwenyekiti wake ambae ni Richard Juma Mkanga wapili kushoto, Wajumbe wanaofuata ni Lusiana Nkusa, Lokaido Sintala, Ambas Selemani na John Daniel.

No comments:

Post a Comment