Wednesday, January 22, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA WATUMISHI WA HOSPITALI KUU YA MKOA KUSKILIZA KERO ZAO KWA AJILI YA KUZIPATIA UFUMBUZI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye kikao na watumishi wa idara ya afya wa hospitali kuu ya Mkoa iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga. Alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kusikiliza kero, malalamiko pamoja na ushauri kwa ajili ya kuboresha huduma na utendaji katika hospitali hiyo. Kero mbalimbali zilitolewa ikiwepo upandishwaji wa vyeo kuchukua mda mrefu, kubadilishiwa muundo wa vyeo na kusababisha kupungua kwa mishara kimakosa, uhaba wa vitendea kazi pamoja na madaktari bingwa wa upasuaji ambapo kwa sasa hamna hata mmoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya kusikiliza kero mbalimbali aliagiza uongozi wa hospitali hiyo kutatua kero zilizo chini ya uwezo wao na zile nyingine kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa kuzishirikisha mamlaka husika. Kushoto ni Mganga Mkuu hospitali ya Mkoa Rukwa Dkt. William Gurisha. Kero nyingi zimeonekana kuibuka kutokana na uhaba wa fedha za OC kutofika kwa wakati na kwa kiwango kilichopangwa. Hata hivyo hospitali hiyo imeonekana kujipanga kutumia vyanzo vya mapato ya ndani kutatua baadhi ya kero hizo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla akifafanua baadhi ya mambo ya kiutawala katika kikao hicho. 
Wajumbe katika kikao hicho.
Mmoja ya wahudumu wa afya akitoa kero yake.

No comments:

Post a Comment