Saturday, January 11, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA ASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA WA KANISA LA KKKT SUMBAWANGA NA KUUNDA DAYOSISI MPYA YA ZIWA TANGANYIKA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa 8 wa kanisa la kiinjili na kilutheri Tanzania KKKT la mjini Sumbawanga ambapo utafanyika uchaguzi Mkuu wa Kanisa hilo na kuzaa Dayosisi mpya ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Katika hotuba yake hiyo aliwaasaviongozi na waumini wa kanisa hilo kuepukana na vitendo vya rushwa katika kuweka uongozi kanisani hapo pamoja na kuepukana na mambo maovu na machafu ikiwemo kudumisha amani ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiimba moja ya wimbo wa maubiri na Baba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga Askofu Damian Kiaruzi wakiwa miongoni mwa wageni waalikwa katika Mkutano huo.
Kwaya ya Kanisa hilo.
Sehemu ya waumini na waalikwa katika Mkutano huo.
Picha ya pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiagana na viongozi wa kanisa hilo na baadhi ya wageni waalikwa.

No comments:

Post a Comment