Tuesday, January 14, 2014

MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA AVAMIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WIILAYA YA NKASI, AWATAKA KUBORESHA MAKUSANYO YA MAPATO YA HALMASHAURI YAO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia baraza kuu la madiwani wa Wilaya ya Nkasi (Full Council) lililokua kwenye kikao cha kujadili na kupitisha bajeti ya fedha ya mwaka 2014/2015 na kupitisha sheria ndogondogo za halmashauri. Katika hotuba yake aliwataka madiwani na viongozi wa halmashauri na wilaya ya Nkasi kushirikiana kwa pamoja na kuweka pembeni itikadi zao katika kuunda vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia kwa kuwekeana mikakati maalum ya makusanyo kwa kila kijiji, kata, tarafa, halmashauri na Wilaya kwa ujumla. Alisema halmshauri hiyo haitaweza kuendelea kwa kuendelea kuwa tegemezi kutoka Serikali kuu na badala yake waongeze makusanyo ya ushuru na mapato yasaididie katika mipango ya kujiendeleza. Kikao hicho kilipitisha bajeti ya Tsh Bilioni 25.4.Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akizungumza katika kikao hicho ambapo alisisitiza juu ya kuboresha na kusimamia upatikanaji wa mapato ya halmashauri ambayo pamoja na mambo mengine yatasaidia katika kuboresha miundombinu ya barabara katika Wilaya hiyo ambayo imekua ndio kilio kikubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Albinus Mugonya.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika kikao hicho. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Peter Mizinga.
Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi waliohudhuria kikao hicho.Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

No comments:

Post a Comment