Wednesday, January 8, 2014

PAMOJA NA VIVUTIO VINGI VINAVYOPATIKANA MKOANI RUKWA, VIPO PIA VIVUTIO VYA KIIKOLOJIA AMBAVYO VINAHITAJI TAFITI ZAIDI KUVIIBUA

Ni jambo la faraja kuwa Mkoa umejaliwa vivutio vingi vya utalii, hasa vile vya ikolojia. Vivutio hivyo vimekuwa havitangazwi kwa sababu ya kutokuwa na tafiti za kutosha. Hali kadhalika kutokana na Mkoa huu kukosa miundombinu ya uhakika hususani ya barabara na umeme.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kapozwa Wilayani Kalambo alipofanya ziara hivi karibuni.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella M. Manyanya (Mb) pamoja na timu ya wataalamu wa Mkoa na Halmashauri wamedhamiria kuviibua vivutio hivyo.  Njia inayotumika kwa sasa ni ile ya kutumia uzoefu wa kuona kwa kulinganisha na vivutio kama hivyo vilivyoonekana maeneo mengine na kuliingizia Taifa lao au mkoa fedha nyingi.  Pia mkoa unatafuta taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi wa maeneo ya Kata na Vijiji, na hivyo kufuatilia kwa karibu taarifa hizo.
Kinachofariji ni kwamba watu wengi hata wa vijijini wanatambua juu ya vivutio hivyo japo kwa sasa havitumiki katika kuvutia watalii.
 
Katika ziara yake aliyoifanya tarehe 4 hadi 5 Januari, 2014, Mkuu huyo wa Mkoa alivutiwa sana na miamba inayozunguka milima ya kipanga inayoambatana na mimea mizuri inayopamba miamba hiyo. 
Eng. Stella Manyanya ameifananisha miamba hiyo na ile aliyoiona katika jimbo la Yunnan China katika mji mdogo Stone Town ambapo ni eneo la kivutio kikubwa sana cha utalii.  Pia katika eneo hilo kuna pango linalosadikiwa kutengeneza njia ya kutokea kijiji jirani cha Samazi. 
Hata hivyo hakuna ambaye ameweza kuhakikisha zaidi ya kufuatilia pangohilo kwa umbali uziozidi mita 30, kutokana na hofu ya mazingira ya sitofahamu ndani ya pango hilo. 
 Mbunge wa jimbo la Kalambo Mh. Josephat Kandege akitoka katika pango lenye njia ya ndani ya  mwamba wa jiwe katika kijiji cha Kipanga Kata ya Kasanga wilaya Kalambo. Njia hiyo inadaiwa kupita chini ya ardhi na kutoka katika kijiji cha jirani cha Samazi kilichopo umbali wa takribani kilometa tisa na kwamba ilitumiwa na wakoloni wa Kijerumani wakati wa ukoloni.

Mkoa unawaalika wataalamu wa utalii ya ikolojia kufanya tafiti zaidi.
 
PICHA NA RAMADHANI JUMA-AFISA HABARI WILAYA YA KALAMBO

No comments:

Post a Comment