Saturday, January 4, 2014

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA WILAYANI NKASI, AKAGUA SHAMBA DARASA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA MAJI MATALA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na uongozi wa Wilaya ya Nkasi alipotembelea shamba la shule ya Msingi Matala ambalo pia linatumika kama shamba darasa ukiwa ni mpango ulioanzishwa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa kusaidia elimu ya kilimo mashuleni na kusaidia upatikani wa chakula kwa wanafunzi. Katika mpango huo kila shule Mkoani Rukwa imetakiwa kuwa shamba ekari zisizopungua tano ambazo zitapatiwa ruzuku ya pembejeo inayotolewa na Serikali na kusimamiwa na afisa ugani wa eneo husika na kuwa shamba la mfano kwa wananchi katika Kilimo bora.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi unaondelea wa mradi wa maji katika kijiji cha Matala Wilayani humo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Matala Wilayani Nkasi jana. Mradi huo unaofadhiliwa na Serikali, mpaka kukamilika kwake utatumia zaidi ya Tshilingi milioni 300. Jumla ya vijiji kumi (10) katika wilaya ya Nkasi vinategemewa kupata maji ya uhakika kutokana na miradi inayoendelea ambapo zaidi ya Tsh. Bilioni tisa zimeshatengwa kukamilisha ujenzi wake. Changamoto zinazoikabili miradi hii ni kuchelewa kwa fedha kutoka Wizara ya maji pamoja na uhaba wa mabomba na viungio vyake kutoka viwandani.
Picha ya pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi jezi Kapteni wa Timu ya Matala FC Filbert Ndiela kama moja ya kampeni zake Mkoani Rukwa kuhamasisha michezo kwa vijana, ujasiriamali na kujituma katika shughuli za maendeleo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta. Katika hotuba yake Injinia Manyanya alitoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia ya kulima kwenye vyanzo vya maji na kuwaomba wananchi kujali afya zao kwa kujitolea kupima VVU na kinamama wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya afya au zahanati.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya hotuba yake na kabla ya kuondoka kwenye mkutano wa hadhara wananchi walimuomba awachezee ngoma yao ya kabila la kifipa ambayo aliitendea haki vilivyo kama anavyoonekana pichani kulia. 
Kijiji cha Matala.

No comments:

Post a Comment