Saturday, March 8, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI RUKWA, WANAWAKE WAASWA KUJIENDELEZA KIELIMU KUSHIKA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI NCHINI

Maadhimisho hayo yalianza kwa maandamano mbalimbali yaliyopita mbele ya meza kuu ambayo mgeni rasmi alikua Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Viongozi mbalimbali wa meza kuu wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya  Nkasi Mhe. Iddi Kimanta (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Maembe (wa pili kushoto) na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Francis Kilawe (wa nne kushoto) wakionyesha ishara ya kupokea maandamano hayo. Wengine kutoka kulia ni Makatibu Tawala wa Wilaya za Nkasi, Kalambo na Sumbawanga.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta (wa nne kushoto) na viongozi wengine wa Serikali Mkoani Rukwa wakipokea maelezo ya bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajasiriamali waliofanya maonyesho ya bidhaa zao katika sherehe hizo. Pamoja na maonyesho hayo huduma za kupima VVU kwa hiyari pia zilitolewa sambamba na michezo mbalimbali na nyimbo za kunogeza sherehe hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta akihutubia hadhara iliyohudhuria maadhimisho hayo ambapo amewataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kujiendeleza kielimu waweze kushika nafasi mbalimbali za uongozi kama walivyofanikiawa viongozi wengine wanawake hapa nchini na barani Afrika. Aliwatolea mfano baadhi ya viongozi hao kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Anna Makinda n.k.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkabidhi Bi Bahati Mgimwa Afisa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Wilaya ya Sumbawanga zawadi mbalimbali zilizotolewa na Dawati la Jinsia Mkoa wa Rukwa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika Kijiji cha Kalambanzite Wilayani Sumbawanga. Zawadi hizo zenye thamani ya shilingi laki tatu ni Sabuni, Sukari, Chumvi na nguo.
Kikundi cha waalimu wakiimba wimbo wa kumsifia na kumtukuza mwanamke. Hakika wimbo wao ulikuwa na msisimko mkubwa kwa washiriki wote wa maadhimisho hayo. 
Kwaya ya wanafunzi shule ya Sekondari Laela wakiimba wimbo wa kumtukuza na kumsifia Mwanamke. Washiriki wa maadhimisho hayo waliguswa na kwaya hii na kupata msisimko wa aina yake jambo ambalo wengi wao walishindwa kuvumilia na kuamua kuwatunza kwa fedha mbalimbali.
Baadhi ya viongozi wanawake wa Serikali na chama Mkoani Rukwa waliotolewa mfano wa mafanikio na Mgeni Rasmi kuweza kuwashawishi wanawake wengine kuiga mfano wao wakiwapigia makofi wanawake wenzao walioshiriki maadhimisho hayo kuwa wanaweza wakiamua. 
Watoto wa kike nao walikuwepo kusherehekea siku yao kwa kubadilishana mawazo ya hapa na pale.

No comments:

Post a Comment