Thursday, March 6, 2014

PICHA MBALIMBALI KUTOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA

 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Christopher Ole Sendeka akichangia mjadala kuhusu vifungu vya kanuni vitakavyotumika katika Bunge Maalum la Katiba.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Democratic Party (DP) MchungajiChristopher Mtikila akitoa hoja yake wakati wa Kikao cha Semina uundwaji wa Kanuni zitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba jana Mjini Dodoma.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati inayoshughulikia uundwaji wa kanuni zitakazoongoza Bunge Maalum la Katiba Bi. Mgeni Juma akisoma baadhi ya vifungu vya kanuni vilivyofanyiwa marekebisho jana Mjini Dodoma.
 
Mweyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba Pandu Ameir Kificho akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Bunge hilo jana Mjini Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akimweleza jambo Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Mohamed Seif Khatib (kulia) Wakati wa Kikao cha Semina uundwaji wa Kanuni zitakazoongoza Bunge Maalum la Katibajana  Mjini Dodoma. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi.PICHA NA HASSAN SILAYO

No comments:

Post a Comment