Thursday, March 13, 2014

SIKU YA UTEPE MWEUPE KITAIFA MKOANI RUKWA, WILAYA YA KALAMBO YACHANGIA VIFUKO (UNITS) 141 YA DAMU SALAMA

Mkazi wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa akichangia damu.
Masanduku yaliyohifadhiwa damu yakiingizwa kwenye gari.


Na Ramadhani Juma - Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo
............................................................................
Wakazi wa wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa wamechangia vifuko 141 vya damu kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto wenye uhitaji katika kampeni ya uchangiaji damu kwa hiari iliyoendeshwa na asasi ya Utepe Mweupe jana mjini Matai na kuhusisha makundi yote ya kijamii wakiwemo baadhi ya wanafunzi wa Sekondari.
Zoezi hilo ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe (White Ribon) yanayofanywa kitaifa Mkoani Rukwa na yanatarajiwa kufikia kilele chake Machi 15 mwaka huu.
Mratibu wa zoezi hilo kitaifa Rose Mlay aliwashukuru wakazi wa wilaya ya Kalambo kwa moyo wa kujitolea kwa ajili kuwasaidia akina mama wajawazito na watoto ambao baadhi yao wamekuwa wakipoteza maisha kwa kukosa damu.
Sherehe za kilele cha maadhimisho hayo zitafanywa katika kata ya Mtowisa wilaya ya Sumbawanga Vijijini Mkoani Rukwa Machi 15 mwaka huu, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mizengo Pinda.

No comments:

Post a Comment