Thursday, April 3, 2014

KATIBU MKUU WA CCM, KINANA ATEMBELEA WANANCHI WA KASANGA,WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na baadhi ya viongozi wa chama Wilaya ya Kalambo,wakikatiza kwenye Ofisi ya CHADEMA,ambayo inadaiwa imefungwa miaka mitatu 3 sasa kwa kushindwa kulipia pango.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka mchanga kwenye mashine ya kufyatulia tofali ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa jengo la CCM,wilayani Kalambo
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akibeba tofali aliyoifyatua,ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa jengo la CCM,wilayani Kalambo
 Wajumbe wakifurahia jambo mara baada ya Ndugu Kinana kuzungumza jambo mbele yao.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe nyumbani kwa Mjumbe wa shina No.1,Bwa.Apolinali Kwidikwa,katika kata ya Kateka,wilayani Kalambo mkoani Rukwa mapema jana jioni.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Matai,katika wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa mapema jana jioni.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu  Kinana akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa kijiji cha Kasanga Wilayani Kalambo jana jioni,kabla ya kufanya mkutano wa hadhara na kuzunguma na wananchi hao mambo mbalimbali ikiwemo Afya,maji,Elimu.Barabara na mengineyo.
 Baadhi ya Wanachi wa kijiji cha Kasanga wilayani Kalambo wakifuatilia mkutano. 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa,Balozi Ally Karume akihutubia mbele ya wananchi wa kijiji cha Kasanga,Wilayani Kalambo mkoani Rukwa mapema jana,wakati wa mkutano wa hadhara.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akila kiapo na  Sehemu ya Wanachama wapya waliojiunga na CCM na kukabidhiwa kadi,ambapo Wanachama wapya 266 wamejiunga na chama hicho katika kata ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
 Sehemu ya Wanachama wapya waliojiunga na CCM na kukabidhiwa kadi na Ndugu Kinana wakila kiapo.Wanachama wapya 266 wamejiunga na chama hicho katika kata ya Kasanga wilayani Kalambo mkoani Rukwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizawadiwa zawadi kutoka kwa akina mama wa kata ya Kasanga,iliopo ndani ya wilaya mpya ya Kalambo,mkoani Rukwa.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Kasanga,iliopo ndani ya wilaya mpya ya Kalambo,mkoani Rukwa mapema jana jioni.Kinana bado yupo Mkoani Rukwa na ziara yake ya kuimarisha chama,kukagua miradi mbalimbali,ikiwemo na kusikiliza kero za wananchi. 
Baadhi ya akina mama wakazi wa kata ya Kasanga wilayani kalambo wakishangilia jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akizungumzia mambo mbalimbali ikiwemo utatuzi wa masuala ya  Afya,Elimu,Barabara na maji.
Waendesha bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuelekea kijiji cha Matai,Makao makuu ya Wilaya ya Kalambo kuendelea na ziara yake ya kuimarisha chama,kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa ya hali ya kisiasa katika wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa mapema jana. (Picha na Jiachie Blog)

No comments:

Post a Comment