Saturday, April 5, 2014

KINANA AAHIDI KUZITAFUTIA UFUMBUZI KERO ZA WAFANYABIASHARA SUMBAWANGA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa Mji wa Sumbawanga, kuhusu matatizo mbalimbali ikiwemo utitiri wa kodi na jinsi wanavyosumbuliwa  na maofisa biashara pamoja na malalamiko yao kuhusu mashine za TRA.Mazungumzo hayo yalifanyika leo katika Jengo la Chama cha Walimu, mjini Sumbawanga.
MfanyabiasharaWillington Kiziba  akilalamika mbele ya Kinana kuhusu kodi nyingi za biasshara na mazao ya kilimo.

 Mfanyabiashara Nobert Mbala akielezea mbele ya Kinana jinsi wanfanyabiashara wanavyonyaswa
 Honory Daud naye akielezea jinsi wanyabishara wanavyonyanyaswa kiasi cha kuichukia Serikali  
Mfanyabiashara Martine Tulo akilalamikia kitendo cha Manispaa kuweka kodi ya Fire wakati wa ununuzi wa viwanja


Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Sabas Katepa akikiri mbele ya Kinana na wafanyabiashara kuhusu mpangilio mbovu wa kodi na malipo ya leseni na kuahidi kuyafanyia maboresho haraka
 Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, naye akikiri mbele ya Kinana kutowashirikisha wafanyabiashara kupanga kodi mbalimbali

Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aeshi Hillal akikubali kuwepo matatizo hayo na kuahidi kusaidiana na Kinana kupata ufumbuzi wa kero hizo ikiwemo ya mashine za TRA
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Emmanuel Kilindu  akitembelea magongo alipokuwa akitoka kwenye mkutano  na wafanyabiashara


Kinana (wa pili kuliai)akiwa na maofisa wengine wa CCM wakitoka kwenye mkutano na wafanyabiashara wa Mji wa Sumbawanga (Picha na Jiachie Blog)

No comments:

Post a Comment