Wednesday, May 28, 2014

MKUU WA KITENGO CHA POLISI JAMII NCHINI NDUGU MICHAEL KAMUHANDA AONANA NA MKUU WA MKOA WA RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kushoto akizungumza na viongozi wa Idara ya Polisi Jamii kutoka Makao Makuu ya jeshi la Polisi wakiongozwa na Mkuu wa kitengo hicho Ndugu Michael Kamuhanda walipofanya ziara ya kikazi Mkoani Rukwa jana tarehe 27 Mei, 2014. Ndugu Kamuhanda alisema kuwa pamoja na mambo mengine wamefika kuangalia kama sera na Ilani ya Chama Tawala CCM inazingatiwa ya kuhakikisha kila makao makuu ya kata kunakuwa na kituo cha Polisi pamoja na askari 15 katika kila kata. Amesema kwa kiwango kikubwa sera hiyo imetekeleza na kwamba jitihada zinaendelea kufanywa ambapo polisi wapya watakaomaliza mafunzo hivi karibuni watapangiwa katika vituo husika.
Ndugu Michael Kamuhanda kushoto akiwa na viongozi wengine kutoka kitengo cha Polisi Jamii makao makuu ya Jeshi la Polisi wakiwa katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ofisini kwake mapema jana.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifurahia jambo na viongozi hao wa jeshi la Polisi kitengo cha Polisi Jamii makao makuu ya jeshi hilo. Wa pili shoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa. Mkuu huyo wa Mkoa amelishukuru jeshi la Polisi nchini kwa kuongeza nguvu katika uslama wa raia kwa kuongeza idadi ya Polisi kufikia 15 katika kila Tarafa sera ambayo ni ya kitaifa, aidha ameliomba jeshi hilo makao makuu kuongeza nguvu kidogo kwa jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa katika ujenzi uanoendelea wa nyumba za makazi za askari wa jeshi hilo.

No comments:

Post a Comment