Sunday, June 8, 2014

SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI ILIVYOADHIMISHWA MKOANI RUKWA

Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katika sherehe za maadhimisho ya wiki ya siku ya Mazingira Duniani Mkoani Rukwa Ndugu Francis Kilawe ambae pia ni Katibu Tawala Mkoa Msaidizi kitengo cha Miundombinu akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu huyo wa Mkoa kwenye sherehe hizo zilizofanyika kimkoa katika shule ya Msingi Msua katika Manispaa ya Sumbawanga tarehe 05 Juni 2014. Katika hotuba yake hiyo aliwataka wadau wote wa mazingira kutunza vyanzo vya maji na kupanda miti kwa wingi katika kuhifadhi mazingira. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ikiwa "CHUKUA HATUA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI".
Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika maadhimisho hayo Ndugu Francis Kilawe akimpa Ndugu Reyo (Kidevu) tuzo ya Rais ya Uhifadhi Mazingira ambayo ni cheti na fedha taslim Tsh. 30,000/=  kwa kuibuka mshindi katika shughuli za uhifadhi wa mazingira na upandaji miti Mkoani Rukwa.
Sehemu ya washiriki wa maadhimisho hayo ambao wengi wao walikua wanafunzi wa shule ya Msingi Msua yalikofanyika maadhimisho hayo.
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Msua katika Manispaa ya Sumbawanga ambao baadhi yao walilazimika kupanda juu ya miti kupata taswira mwanana ya maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment