Wednesday, June 4, 2014

WILAYA YA KALAMBO - RUKWA YAIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

IMG_2477MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa Godfrey Sichona akikabidhi sare kwa mratibu wa Elimu wa Kata ya Legezamwendo ili zigawanywe kwa wanafunzi yatima na wanaoishi katika mazingira magumu. PICHA KWA HISANI YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO
IMG_2467
MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa Godfrey Sichona (mwenye suti) na Makamu wake Faustine Mwanisenga wakikagua gitaa wakati walipokabidhi vifaa vya muziki kwa vikundi viwili vya Kwaya katika Kata za Legezamwendo na Mambwenkoswe ili visaidie mapambano dhidi ya UKIMWI kwa njia ya nyimbo wilayani humo Kulia ni mratibu wa UKIMWI  wa wilaya hiyo Mariam Kimashi.
PICHA KWA HISANI YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA KALAMBO
NA RAMADHANI JUMA
OFISI YA MKURUGENZI-KALAMBO
 
OFISI ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa kupitia kitengo cha UKIMWI kimetumia zaidi ya shilingi milioni 8.5 kwa ajili ya kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo katika wilaya hiyo.
 
Fedha hizo zimetumika kuwanunulia wanafunzi yatima wanaoishi katika mazingira magumu sare za shule, viatu pamoja vifaa vya kujifunzia ikiwemo madaftari na kalamu, ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Godfrey Sichona alikabidhi kwa walengwa kwa niaba ya Halmashauri.
 
Pia Halmashauri hiyo imenunua vifaa vya muziki kwa ajili ya vikundi viwili vya Sayuni kilichopo kata ya Legezamwendo na Sayuni cha Kata ya Mambwenkoswe ili vihamasishe wananchi kujikinga na ugonjwa huo.
 
Baadhi ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Halmashauri hiyo ya Kalambo ni gitaa tatu kila kikundi, spika, maikrofoni, genereta pamoja na vifaa vingine vya umeme.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, mwenyekiti huyo aliwakumbusha wakazi wa wilaya ya Kalambo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla kuwa, mapambano dhidi ya UKIMWI sio ya serikali pekee bali ni jukumu la kila mwanajamii zikiwezo taasisi za dini.
 
Naye mwenyekiti  wa kamati ya Kudhibiti UKIMWI wilaya ya Kalambo Faustine Mwanisenga aliwataka wanavikundi waliopatiwa msaada wa vifaa vya muziki na Halmashauri hiyi kuvitunza na kuvitumia vizuri ili kufikia malengo yaliyokusudiwa

No comments:

Post a Comment