Monday, February 9, 2015

KIKAO KATI YA MKUU WA MKOA WA RUKWA NA UMOJA WA WAMILIKI NA WAENDESHA DALADALA NA TAXI MJINI SUMBAWANGA KUSIKILIZA KERO ZAO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Umoja wa Wamiliki na Waendesha Daladala na Taxi wa Mjini Sumbawanga tarehe 09/02/2015 kufuatia ombi la umoja huo kuwasilisha kero zao ambapo kubwa ikiwa utaratibu wa Waendesha Bajaji na Bodaboda kutokua na vituo maalum hivyo kuharibu biashara yao ambayo ina vituo maalum. Kufuatia kero hiyo Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kuifanyia kazi na kuwaasa umoja huo kuwa na subira wakati kero hiyo ikiwa inafanyiwa kazi na kuwa mstari wa mbele katika kuleta amani katika Mkoa wa Rukwa.
 Mmoja wa Madereva taxi aliyefahamika kwa jina moja la Masawe akieleza kero mbali mbali wanazokabiliana nazo kutoka kwa wafanyabiashara wa bodaboda na bajaji Mjini Sumbawanga. (Picha na Frank Maten - DPS)


No comments:

Post a Comment