Sunday, February 22, 2015

MKAKATI WA KUENDELEZA ENEO LA MAPOROMOKO YA MTO KALAMBO MKOANI RUKWA WACHUKUA SURA MPYA, MKUU WA MKOA HUO AKAGUA UJENZI WA GETI LA KUINGILIA KATIKA MAPOROMOKO HAYO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa baadhi ya maelekezo kwa fundi anaejenga geti litakalotumika kutoza ushuru kwa watalii wa nje na wa ndani watakaofika kuona maporomoko ya mto Kalambo (Kalambo Falls) ambayo ni maporomoko ya pili kwa ukubwa barani Afrika. Maporomoko hayo ambayo yapo Mkoani Rukwa mpakani na nchi jirani ya Zambia yamekuwa yakinufaisha zaidi upande Zambia ambao wamejenga miundombinu kadhaa kuwawezesha na kuwavutia wanaofika kuona maporomoko hayo. Mto unaotengeneza maporomoko hayo upo nchini Tanzania na hata muoenekano mzuri unapatikana kutokea upande wa Tanzania. Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ameamua kusimamia kidete kuhakikisha miundombinu kadhaa inajengwa katika eneo hilo la maporomoko ili rasilimali hiyo adimu iweze kutambulilaka na kutoa mchango wa kiuchumi kwa taifa na Halmashauri husika ya Wilaya ya Kalambo.
Jengo ambalo litatumika kama geti la kuingilia katika maporomoko ya Mto Kalambo na ambalo pia litatumika kama eneo la kutoza ushuru kabla ya watalii kuingia kushuhudia maporomoko hayo likiwa katika hatua ya ujenzi wa awali.
 Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Hamza Temba akifurahia maajabu ya maporomoko ya Mto Kalambo.
 Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Ndugu Frank Maten(Kulia) na baadhi ya watalii wa ndani waliofika kuangalia maporomoko hayo wakifurahia maumbile ya asili ya eneo hilo. 
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment