Friday, February 13, 2015

MKUU WA MKOA WA RUKWA AFUNGA MAFUNZO YA SIKU MBILI YALIYOANDALIWA NA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA TANZANIA KWA KAMATI ZA MAADILI MIKOA YA RUKWA NA KATAVI LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisoma hotuba ya kufunga mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania kwa kamati za maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi na kufanyika Mjini Sumbawanga tarehe 12-13 Februari 2015. Katika hotuba yake hiyo ameiomba Serikali kutenga fedha ya kutosha ili mafunzo kama hayo yaweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa ustawi wa Sheria na Haki nchini. Mafunzo hayo ni katika mkakati wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania kuimarisha tume za maadili nchini kusaidia maadili kwa watumishi wa Mahakama nchini. Kushoto ni Jaji Ferdinand Wambali muwezeshaji wa mafunzo hayo ambae ni Jaji wa Mahakama Kuu na Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto .
Bi Enzel Mtei ambae ni miongoni mwa wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Tume ya Mahakama Tanzania akimuwakilisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama akizungumza muda mfupi kabla ya kuhitimishwa mafunzo hayo. Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa katika mafunzo hayo kwa wanakamati; Mihimili yote ya dola nchini ifanye kazi kwa pamoja ili kutoa haki kwa wakati, Amri halali itakayotolewa namamlaka husika iheshimiwe kuleta usawa wa kisheria nchini na Mahakimu pamoja na wadau wengine wa sheria wawe mfano kwa maadili bora katika jamii.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa katikati na wajumbe wengine wakifuatilia mafunzo hayo.
 Wajumbe wa Kamati ya maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment