Thursday, February 12, 2015

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA VIONGOZI NA WAJUMBE WA MFUKO WA CHANGAMOTO ZA MILLENIA (MCAT), AWAPONGEZA KWA KAZI NZURI YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) wakiongozwa na mwenyekiti wake ambae pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi  Dr. Servaciaus Likwelile (kulia)  ofisini kwake leo tarehe 12 Februari 2015. Katika salam zake ameishukuru Serikali na mfuko huo kwa kazi nzuri inayofanyika Mkoani Rukwa na taifa kwa ujumla hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami, Pamoja na hayo ameiomba Serikali na wafadhili wa MCC kusaidia pia katika ujenzi wa barabara muhim za Wampembe iliyopo Wilaya ya Nkasi, barabara ya bondeni kwa ajili ya kuunganisha ukanda wa bonde la Ziwa Rukwa unaoongoza kwa uzalishaji wa mpunga na Mikoa ya Katavi na Mbeya, barabara ya Kasesha kwa ajili ya kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Zambia na barabara ya kuelekea Kalambo Falls yalipo maporomoko ya Mto Kalambo ambayo ni ya pili kwa urefu barani Afrika.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (kulia) akiendesha kikao ofisini kwake mapema leo tarehe 12 Februari 2015 kati yake na viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) .
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa zawadi ya kanga kwa Katibu Mkuu Wizara ya fedha na uchumi Dr. Servaciaus Likwelile pamoja na viongozi wengine na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T), Kanga hiyo ni ishara ya mafanikio ya miaka 40 ya Mkoa wa Rukwa 1974-2014.    
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (kulia) alipata fursa ya kuwaalika viongozi na wajumbe wa Mfuko wa Changamoto za Millenia Tanzania (MCA-T) kwa ajili ya chakula cha usiku walipowasili Mkoani Rukwa tarehe 11 Februari 2015. Anaechukua chakula ni Mwenyekiti wa mfuko huo ambae pia ni Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Uchumi Dr. Servaciaus Likwelile.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment