Wednesday, February 18, 2015

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA (RCC) LEOMkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akiwa anasoma hotuba ya ufunguzi wa kikao hicho leo tarehe 18 Februari 2015 katika ukumbi wa RDC Mjini Sumbawanga. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Kimanta na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Methew Sedoyyeka. Kulia kwa Mkuu huyo wa Mkoa ni Katibu Tawala Mkoa huo Ndugu Smythies Pangisa.

 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya ufunguzi wa kikao hicho. Kuli ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Hyporatus Matete.
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho ambao ni wabunge wa Mkoa wa Rukwa. Kutoka kulia ni Mhe. Kandege Jimbo la Kalambo, Mhe. Malocha Jimbo la Kwela na Mhe. Ally Kesi Jimbo la Nkasi Kusini.
 Sehemu ya wajumbe na wagei waalikwa katika kikao hicho.
Meneja wa Idara za Serikali na Ofisi za Balozi NSSF Bi. Rehema H. Chuma akitoa mada juu shughuli na mafao ya shirika hilo katika kikao hicho. Aliwaasa viongozi na wanasiasa kuhamasisha wananchi wajiunge katika vikundi mbalimbali watambuliwe na waweza kunufaika na mpango wa mafao wa NSSF kwa makundi maalum, mfano wavuvi, wakulima na wafugaji. Amewataka pia wachangiaji wa mfuko huo ambao ni watumishi pindi wanapohama watoe taarifa zao kurahisisha ufuatiliaji wa mafao yao.
 Meneja wa Idara za Serikali na Ofisi za Balozi NSSF Bi. Rehema H. Chuma akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kitabu Muongozo wa Utendaji wa NSSF muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao hicho. Kulia ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Rukwa Ndugu William Lutambi.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa wa kikao hicho.
 Wajumbe na waalikwa wa kikao hicho.
 Sehemu ya waalikwa katika kikao hicho.
Baadhi ya waalikwa na watoa mada katika kikao hicho.

No comments:

Post a Comment