Saturday, February 14, 2015

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AKABIDHI KATIBA PENDEKEZWA KWA WILAYA ZOTE MKOANI RUKWA LEO


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akimkabidhi Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Bi. Mapinduzi Severian Katiba pendekezwa leo tarehe 14 Februari 2015 kwa niaba ya wananchi wa Wilaya hiyo ambao watapata fursa ya kuiona na kuisoma kwa ajili ya kuipigia kura ya maoni mwezi Aprili mwaka huu. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha muimbaji wa kikundi cha ngoma za asili ya Kanondo Katiba pendekezwa katika hafla fupi ya kukabidhi Katiba hiyo iliyofanyika katika Wilaya ya Kalambo. \Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akimuonyesha Ndugu Mulele Mulenda Mwanaukawa aliyeshiriki hafla hiyo fupi ya kukabidhi Katiba pendekezwa kwa niaba ya Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Kalambo sehemu ya vifungu vya katiba pendekezwa ambavyo vipo na vilikuwepo kwenye rasimu ya Katiba ya Jaji J. Warioba ambpo ni kinyume na inavyodaiwa na UKAWA kuwa vimechakachuliwa.
 Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo, Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kalambo muda mfupi baada ya kukabidhi Katiba pendekezwa. Aliwataka wananchi hao kujitokeza kwa wingi mwezi April kwa ajili ya kuipigia kura  katiba hiyo na kutopotoshwa kwa namna yeyote ile na watu wasioitakia mema nchi yao. Alisema kuwa katiba hiyo ni nzuri kwani imegusa maslahi ya watanzania wote na ustawi wa taifa kwa ujumla. 

Baadhi ya wananchi wakionekana kujifunika na mwanvuli kufuatia mvua iliyokua ikinyesha mwishoni mwa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment