Monday, February 23, 2015

WAWAKILISHI KUTOKA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM WAONANA NA MKUU WA MKOA WA RUKWA KUJADILI UANZISHWAJI WA CHUO HICHO MKOANI RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wawakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema leo tarehe 23 Februari 2015 ofisini kwake kujadili mchakato wa uanzishaji wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mkoani Rukwa. Chuo Kikuu hicho kitaleta maombi maalum kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuomba kupatiwa kambi ya Kianda iliyokuwa ikitumiwa na Kampuni ya Aasleaf Bam International iliyokuwa ikijenga barabara ya Laela - Sumbawanga kwa kiwango cha lami. Kwa upande wa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa unaona kuna haja kubwa ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Mkoani humo kuweka chachu ya elimu na kusogeza huduma hiyo muhim zaidi kwa wananchi. Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ni Katibu Tawala Mkoa huo Ndugu Smythies Pangisa. 
Dkt. Joseph Kihedu ambaye ni muhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema amefurahishwa na muamko wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya elimu pamoja na kiu yao kubwa ya kuona Mkoa unakua na Chuo Kikuu. Alisema kuwa endapo Chuo Kikuu hicho kitapewa maeneo hayo bila shaka hakitasita kuanzisha Tawi  la Chuo hicho Mkoani Rukwa mbapo itakua ni fursa kubwa kwa chuo hicho kujitanua zaidi katika kutoa elimu yenye ubora nchini. Kutoka kushoto ni wawakilishi wengine kutoka chuo hicho ambao ni Ndugu Michael John na Bi. Brenda Kazimili. 

Majadiliano yakiwa yanaendelea. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya alisema Serikali ya Mkoa haitosita kutoa ushirikiano wa taasisi yeyote ya elimu ya juu ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye lengo la kuwekeza katika elimu Mkoani Rukwa. Amekitaka Chuo Kikuu hicho cha Dar es Salaam kuendelea na nia yake ya kuomba maeneo hayo na kusema kuwa Serikali ya Mkoa itatoa majibu sahihi kwa kile kitakachowezekana.

No comments:

Post a Comment