Sunday, March 1, 2015

MATUKIO KATIKA HAFLA YA KUMBUKIZI YA MCHANGO WA HAYATI RASHID MFAUME KAWAWA KWA TAIFA LA TANZANIA MKOANI RUVUMA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Said Mwambungu akisoma hotuba ya ufunguzi wa hafla ya kumbukizi ya mchango wa hayati Rashid Mfaume Kawawa kwa taifa la Tanzania iliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Songea Mkoani Ruvuma tarehe 26/02/2015, Kaulimbiu ya Kumbukizi hiyo ikiwa Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Simba wa Vita Mzalendo aliyetukuka. Hafla hiyo inakwenda sambasamba na tamasha la kumbukizi ya miaka 110 ya mashujaa wa vita ya majimaji.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa mchango wake katika hafla hiyo. Alitoa rai kwa Mamlaka husika kusaidia habari na simulizi za Uzalendo wa Hayati Mfaume Kawawa kuwafikia wananchi wengi zaidi waweze kujifunza uzalendo kwa nchi yao.
Mwanasiasa Mkongwe nchini Ndugu Kingunge Ngopmbare Mwiru akitoa ushuhuda wa Uzalendo alokua nao Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa enzi za uhai wake. Kwa mujibu wa Ndugu Kingunge wawili hawa walifanya kazi pamoja na pia walikuwa ni marafiki waliofahamiana kwenye harakati za vyama vya wafanyakazi na siasa za ukombozi wa Tanganyika hadi kupata Uhuru. Alimuelezea kuwa mtu wa ajabu ambaye alikubali mabadiliko bila kinyongo chochote hata kama alikua akishushwa kutoka nafasi ya juu kwenda ya chini aliipokea bila manung'uniko yeyote, alielezewa pia kuwa kuwa Kiongozi wa pekee aliyekuwa tayari kupokea lawama kwa niaba ya viongozi wengine wa chama na Serikali akiwemo Baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
Dkt. Magoti, Mstaafu aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Mwl. Nyerere Kigamboni ambae pia ni Muandishi wa Kitabu cha Historia ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa akielezea historia ya Hayati Dkt. Kawawa wakati wa uhai wake. 
 Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo ambapo pia walikuepo watoto, ndugu na jamaa wa karibu wa Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa.
 Alhaj Mustafa Songambele Mwanasiasa Mkongwe Mkoani Ruvuma ambaye sasa ana umri wa miaka 90 akichangia katika haflka hiyo.
Mwanasiasa mkongwe Mkoani Ruvuma Alhaj Mustafa Songambele (90) kushoto akisalimiana na Mwanasiasa Mkongwe nchini Ndugu Kingunge Ngombare Mwiru muda mfupi baada ya uzinduzi wa hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment