Saturday, May 23, 2015

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AONGOZA KIKAO CHA DHARURA CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA RCC NA KUPITISHA MAPENDEKEZO YA KUANZISHA MAJIMBO MAWILI MAPYA YA UCHAGUZI KATIKA WILAYA ZA SUMBAWANGA NA KALAMBO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akizungumza wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kujadili na kufanya uamuzi wa kuanzisha majimbo mapya ya uchaguzi katika wilaya ya Sumbawanga na Kalambo leo tarehe 23 Mei 2015. Kikao hicho kimeridhia mapendekezo hayo ya Halmashauuri husika baada ya kukidhi vigezo ambapo yatapelekwa ngazi za juu kwa uamiuzi zaidi. 

Majimbo hayo yatazaliwa katika majimbo yaliyopo hivi sasa ambapo kwa jimbo la Kwela ambalo lipo katika Wilaya ya Sumbawanga litazaa jimbo la Ziwa Rukwa baada ya kukidhi vigezo vyote vilivyowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi ikiwemo ya idadi ya watu na ukubwa wa jografia. Kwa upande wa jimbo la Kalambo ambalo lipo katika Wilaya ya Kalambo linatarajiwa kuzaa Jimbo jingine la Mambwe. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa taarifa iliyopokelewa na ofisi yake kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya maelekezo ya kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo ya Uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya na Kushoto ni muwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Clemence Bakuli ambaye ni Katibu Mwenezi wa Chama hicho Mkoa.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akifafanua jambo katika kikao hicho. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa wa kikao hicho.
 Sehemu ya wajumbe na waalikwa katika kikao hicho.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUANZA RASMI KESHO JUMAPILI MKOANI RUKWA

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 23 Mei 2015  kuelezea juu zoezi la uandikishiaji wa Wananchi kwenye daftari la kudumu la Mpigakura litakaloanza rasmi kesho tarehe 24 Mei 2015 Mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Mkutano na waandishi wa habari ukiwa unaendelea. Kwa taarifa kamili SOMA HAPA CHINI:-

Friday, May 22, 2015

MKUU WA MKOA WA RUKWA ENG. STELLA MANYANYA AONANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA JIANGXI KUTOKA CHINA INAYOJENGA BARABARA YA LAMI MKOANI RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa Kampuni  ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China ikiongozwa na Mtendaji Mkuu Eng. Zhu Chunhua wa pili kulia  ofisini kwake leo tarehe22/05/2015. Kampuni hiyo inajenga barabara ya lami kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Katavi katika mradi wa Sumbawanga-Kanazi (KM 75). Mkuu huyo wa Mkoa ameipongeza kampuni hiyo kwa ushirikiano wake mzuri na uongozi wa Mkoa katika shughuli zake za ujenzi wa barabara hiyo.
 Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akiongoza zoezi la utambulisho wa wageni na wenyeji katika kikao hicho.
Mtendaji Mkuu  wa Kampuni  ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua wa pili kulia akizungumza katika kikao hicho ambapo ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano unaowapa katika kufanikisha ujenzi wa barabara ya lami ya Sumbawanga - Kanazi, aliongeza kuwa kampuni yake ipo tayari kufanya kazi zingine mbalimbali Mkoani Rukwa ikiwepo ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji taka pamoja na kuwekeza katika eneo la ufugaji. 
 Mtendaji Mkuu  wa Kampuni  ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua akimkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya walipomtembelea Ofisini kwake leo. Barabara ya Lami ya Sumbawanga - Kanazi - Namanyere - Kizi - Kibaoni inajengwa kwa fedha za Serikali ya Tanzania na ujenzi wake bado unaendelea.
 Picha ya pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya kulia akiteta jambo na Mtendaji Mkuu  wa Kampuni  ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China Eng. Zhu Chunhua muda mfupi kabla ya kuagana mapema leo.

Thursday, May 21, 2015

MAOFISA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA WAONYWA KUTOJIHUSISHA NA SIASA WAKATI WA KAZI

Na Gurian Adolf, Sumbawanga (Pembezoni Kabisa Blog)


SERIKALI wilayani Sumbawanga imewataka maafisa uandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura kutoingiza itikadi za kisiasa wakati wa uandikishaji wapiga kura kwani kufanya hivyo kunaweza kuhathiri zoezi hilo na baadhi ya watu wakakosa fursa hiyo kitu ambacho ni kuwakosea haki.
Katibu tawala wilaya ya Sumbawanga, Kisasila Masalu alisema hayo jana wakati akifungua semina ya siku mbili kwa maafisa uandikishaji Manispaa ya Sumbawanga yanayofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo mjini hapa.

‘’ Msiingize siasa katika jambo hili kama mtu ana itikadi zake za kisiasa haziweke kando kwani mkionyesha itikadi zenu kuna baadhi ya watu mtawakatisha tamaa ya kuja kujiandikisha kitu ambacho sio sahihi, pia hakikisheni mnafanya kazi hiyo kwa weledi wa hali ya juu, ili kuepuka malalamiko yasiyo ya lazima,maana haitakuwa sawa baadhi ya wapigakura waliofika kujiandikisha wasipoona majina yao kwenye daftali hilo’’……alisema. 


Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Sumbawanga Rozaria Mugissa akiwaapisha maafisa wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura manispaa ya Sumbawanga.

Alisema kuwa huo ni mfumo mpya wa Biometric Voters Registration(BVR) ambao unatumika kwa mara ya kwanza hapa nchini hivyo wanapaswa kujifunza kwa bidii ili wauelewe ambapo zoezi litakapo anza usiwasumbue na kuharibu kazi hiyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi afungue mafunzo hayo mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, Hamid Njovu alisema kwa mafunzo hayo yatafanyika kwa siku mbili ambapo maafisa uandikisha watajengewa uwezo wa namna ya kufanya kazi hiyo.

Alisema ni jukumu lao pia kuhakikisha wanahamasisha ili wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwani huu ni uandikisha mpya kwakuwa unatumika mfumo mpya ambapo vitambulisho vya mpiga kura vilivyotumika katika uchaguzi mkuu uliopita havitatumika.
Naye, Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Sumbawanga Rozaria Mugissa mara baada ya kuwaapisha waandikishaji hao aliwaasa wafanye kazi hiyo kwa uadilifu mkubwa na kutojihusisha vitendo vyovyote vitakavyosababisha kukwamisha zoezi hilo.