Tuesday, June 23, 2015

ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUKAMILIKA LEO MKOANI RUKWA

 Zoezi la uandikishaji likiwa linaendelea katika kituo cha Katandala "A" kilichopo katika jingo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mjini Sumbawanga tarehe 22 Juni 2015. Zoezi hilo linategemewa kukamilika leo tarehe 23 Juni 2015.

Thursday, June 18, 2015

MATUKIO KATIKA PICHA KWENYE HAFLA YA KUMUAGA RAS TANGA NA KUMKARIBISHA RAS RUKWA KATIKA UKUMBI WA KANYAU SUMBAWANGA MJINI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisalimiana na Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa sasa Mkoa wa Tanga Alhaj Salum Chima  muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kumuaga Ndugu Chima na kumkaribisha Ndugu Smythies Pangisa (katikati) aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara sasa Mkoa wa Rukwa. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 13 Juni 2015 katika ukumbi wa Kanyau Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya hafla hiyo ambaye pia ni Meneja wa SIDO Mkoa wa Rukwa Ndugu Martin Chang'a akitoa salam za utangulizi katika hafla hiyo.
Meza Kuu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza katika hafla hiyo. Aliwaasa watumishi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na ubunifu mkubwa na kwamba  ndiyo siri pekee ya mafanikio katika utendaji wao wa kazi.  
Katika hali isiyotegemewa na wengi Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Alhaj Salum Chima "Muagwa" alitoa zawadi ya machungwa kutoka Tanga ambayo yaligawiwa kwa washiriki wote wa hafla hiyo kama inavyoonekana pichani.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa katika hafla hiyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akizungumza katika hafla hiyo. Kabla ya hapo alikua Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Alhaj Salum Chima wa pili kushoto akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya kinyaturu na baadhi ya wanakikundi wa ngoma hiyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Alhaj Chima na Mkoa wa Rukwa Ndugu Pangisa wakipokea zawadi kutoka kwa Watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
Washiriki wote katika hafla hiyo walipata fursa ya kupeana mikono na Makatibu Tawala hao wa Mkoa wa Tanga na Rukwa.
Watumishi waliofanya kazi kwa karibu zaidi na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Alhaj Salum Chima wakikabidhi zawadi zao.
Picha ya Pamoja kati ya wageni wa meza kuu na wakuu wa idara Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa.