Tuesday, June 28, 2016

Mkuu wa Mkoa aahidi kutembelea shule zote za Rukwa kuangalia ukamilifu wa madawati

Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameahidi kugawana na wafanyakazi wake wa Ofisi ya Mkoa kutembelea Shule zote kuhakiki ukamilifu wa madawati katika Halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa.

Ametoa ahadi hiyo alipotembelea katika ofisi za Halamashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ili kuona maendeleo na juhudi zinazofanywa na Halmashauri hiyo katika kutekeleza agizo la Rais D. John Pombe Magufuli la kutotaka kuona mwanafunzi anakaa chini.

Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa Maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu juu ya aina ya madawati yanayofaa kwa wanafunzi

Mkuu wa Mkoa alionyesha wasiwasi juu ya ukamilifu wa Madawati hadi kufikia tarehe 30, Juni 2016 na alisema “Sifikirii kwamba mpaka June kama mnaweza kutimiza agizo la Rais” 

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ina jumla ya shule za Msingi za seriakali 55 na Sekondari 17, zenye upungufu wa madawati 5,142 kwa shule za Sekondari na Msingi huku asilimia 99 ya uhitaji huo ni katika shule za Msingi za Manispaa hiyo.

Afisa Elimu Msingi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndg Mwashusa akisoma taarifa fupi ya hali ya madawati katika Halmashauri ya Manispaa ya  Sumbawanga.
Mchumi wa Manispaa wa Sumbawanga Saad Mtambule alisema kuwa changamoto kubwa ni ukosefu wa fedha katika kufanikisha hili na Mvua nyingi zilizonyesha mwezi Februari hadi Aprili zilisababisha mbao kutokauka mapema.


Lakini pamoja na Hayo Ng. Mtambule alisema “Pamoja na Changamoto hizo kuna Jitihada kadhaa ambazo tunazifanya ili kukamilisha zoezi ikiwemo kupasua mbao katika msitu uliyopo kwenye baabara ya kwenda Kasanga kwa kibali cha TANROAD na pia kuendelea kupasua mbao katika miti iliyopo mashuleni  na kuwashawishi wadau wa maendeleo kuchangia” 


(Kutoka Kulia) Mkuu wa Mkoa wa Ruwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akifuatiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mh. Justin Malisawe na Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Hamid Njovu.

No comments:

Post a Comment