Tuesday, June 28, 2016

Mkuu wa Mkoa aahidi kuufatilia Uwanja wa ndege wa Sumbawanga

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen
“Nimetembelea ili kuona juhudi zinazofanyika kwani, watu wengi wanahitaji hii huduma, sababu kukiwa na uwanja wa ndege unaofanya kazi mambo mengi yatafunguka, kuna utalii kIpili na shemu nyingine,”Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alisema.

Mkuu wa Mkoa aliweka angalizo kuwa watu waendlee kusubiri kuona nini kitajiri katika Bunge huko Dodoma kuhusiana na hatma ya Uwanja huo na kuongeza kuwa yupo tayari kufunga safari hadi kwa waziri wa wizara husika ili kulitafutia ufumbuzi suala hili.

“Niko Tayari kwenda jwa waziri wa Ujenzi ili kulitafutia ufumbuzi suala hili,” Mkuu wa Mkoa alisisitiza.

Mkuu wa Mkoa pia alitoa agizo kwa wafanyakazi wa Uwanja wa ndege wa Sumbawanga kuweka vibao na alama zinazoonyesha kuwa ni Marufuku watu waendao kwa miguu na baiskeli kupita kwenye uwanja huo lakini pia hata wale wanaotumia vyombo vya moto kama vile Pikipiki, Bodaboda na magari.

“Sheria Zifuatwe na mabango yawekwe ili watu wasitumie uwanja kama njia ya kwenda kwa miguu” Mkuu wa Mkoa aliagiza.

Kiwanja kipo daraja la 3c chenye miundombinu inayoruhusu kutua na kuruka kwa ndege zenye uzito usiozidi tani 20 barabara ya kuruka na kutua kwa ndege “Runway” katika kiwanja ni ya changaraw yenye urefu wa mts 1600 na upana wa mts 30 chenye kuhudumia ndege za abiria, ndege za kukodi “charter flights”pamoja na ndege za serikali na muda mwingine huhudumia jamii.

Kutokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi katika Mkoa wa Rukwa safari za ndege zimetoka 57 kwa mwaka 2002 hadi kufikia safari 260 kwa mwaka 2013 na idadi ya abiria kutoka 122 mwaka 2002 hadi kufikia 1131 mwaka 2013.
Meneja wa Uwanja wa ndege wa Manispaa ya Sumbawanga Sandali Issa Kaisi akisoma taarifa fupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (Hayupo pichani)

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisalimiana na maafisa usalama wa uwanja huo wakati alipotembelea uwanja wa ndege wa Mji wa Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisaini katika kitabu cha wageni katika ofisi za Uwanja wa ndege wa mji wa Sumbawanga. 


No comments:

Post a Comment