Monday, June 27, 2016

Mkuu wa Mkoa aahidi kuwanunulia Uniform Wanafunzi wa Shule maalum ya msingi


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimpa mkono mwanafunzi asiyeona Salum Shabani wakati alipofanya Ziara katika Shule hiyo maalum kwaajili ya wasioona, wenye uoni hafifu na pia wenye ulemavu wa ngozi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameahidi kuwanunulia uniform mpya wanafunzi watano wa darasa la saba wa Shule maalum ya wasioona Malangali iliyopo mjini Sumbawanga baada ya kufanya Ziara Katika shule hiyo kujua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimpa mkono mwanafunzi asiyeona Daniel wakati alipofanya Ziara katika Shule hiyo maalum kwaajili ya wasioona, wenye uoni hafifu na pia wenye ulemavu wa ngozi.

Mkuu wa Mkoa alichukua maamuzi hayo baada ya kuwaona wanafunzi hao wakiwa katika Uniform ambazo haziridhishi kiusafi ambapo wanafunzi hao wote ni wavulana, ili kuweza kuweka usawa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Mathew Sedoyyeka aliamua kuwauliza wasichana nawao walijibu kuwa hawana shida kwa wakati huu.

Shule maalum ya wasioona Malangali ilifunguliwa rasmi tarehe 8, Agosti, 1998 na Rais wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa. Shule ilijengwa na wamishionari na kanisa katoliki toka nchini Ujerumani, Chini ya usimamizi wa Padri Lukewell na kusajiliwa 2003.

Lengo kubwa la kujengwa kwa shule hii ilikuwa ni kutengeneza fursa kwa walemavu wasioona na kupata haki ya msingi ya elimu bora kama ilivyo kwa watoto wengine wasio na ulemavu.
Shule ya Msingi Malangali inasajili wanafunzi kutoka nchi nzima na mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi wasioona na wenye uoni hafifu 52 pamoja na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi 37 na kufanya Jumla ya wanafunzi 89 na waalimu 11.
Wanafunzi wasichana wa Darasa la Saba katika Shule maalum ya MsingiMalangali walipokuwa Darasani wakati Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alipokuwa Napita kuwasalimia.

Shule ya Msingi Malangali haina upungufu wa madawati ila kuna changamoto mbalimbali ambazo shule imekuwa ikijitahidi kukabiliana nazo ikiwemo upungufu wa madarasa manne , vifaa muhimu vya kujifunzia na kufundishia kama vile mashine za kuandikia maandishi ya wasioona na karatasi maalum, ukosefu wa bweni la wanawake na upungufu wa nyumba za walimu na watumishi.

Katika kukabiliana na changamoto hizo shule imefanya jitihada za kuweza kujikwamua ambapo ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeshaainisha miradi miwili yaani ujenzi wa madarasa mawili pamoja na uzio kwa mwaka wa Fedha 2016/2017, shule imekamilisha mazungumzo na wahisani juu ya ununuzi wa gari mpyalenye thamani ya shilingi milioni 22. Na pia mkuu was hue amefanya mazungumzo na wahisani kutoka Ujerumani na wamekubali kuipatia shule Kompyuta 31, 20 ni Desktop na 11 Laptop.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Nestory Mpendakazi akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen namna Printa ya karatasi za nukta Nundu inavyofanya kazi.
Pamoja na jitihada hizo shule imeomba kupewa silaha za moto ili kujilinda kulingana na hali halisi ya mazingira ya shule kwa usalama wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi pamoja na mali za shule.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akipokea maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule maalum ya msingi Malangali katika Bweni la muda la wasichana.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akipokea maelezo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule maalum ya msingi Malangali katika Bweni la  wavulana
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (alieshika kitabu) akiulizia aina ya vitabu ambavyo wanavitumia kila siku katika masomo yao wanafunzi hao wasioona na wenye uoni hafifu .

No comments:

Post a Comment