Tuesday, June 28, 2016

Mkuu wa Mkoa aifundisha SIDO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamaishna Mstaafu Zelote Stephen ametaka shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) kuangalia mahitaji ya wananchi wengi kwa wakati huo ndipo waweze kutengeneza bidhaa zao kulingana na mahitaji hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamaishna Mstaafu Zelote Stephen akiangalia ngozi inayotengenezwa na wajasiriamali wa SIDO na kutengeneza viatu.
Mkuu wa Mkoa alisema kuwa kwa kufanya hivyo kutarahisisha kupata soko ndani ya Mkoa, Tanzania na hata nje ya nchi. “angalieni wananchi wanataka nini kwa kufanya utafiti ndipo mzalishe wanachohitaji ili kupata soko la bidhaa zenu,” alisema hayo alipotembelea shirika hilo ili kutathmini mipango yeke ya kimaendeleo katika Mkoa wa Rukwa.

Ofisi ya SIDO Mkoa wa Rukwa ilifunguliwa mwaka 1975 na mpaka sasa ina wafanyakazi wa kudumu 10 na shirika linatoa huduma mbalimbali ikiwemo mafunzo ya biashara, huduma za ugani pamoja na kuendeleza teknolojia kama kutengeneza sabuni nakadhalika.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamaishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa maelekezo.
Pamoja na kutoa huduma hizo SIDO wamekuwa na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo kama vile wananchi kuwa na mwamko mdogo katika kushuriki mafunzo mbalimbali yanayotolewa na SIDO na pia wananchi kuchelewa kurudisha mikopo mpaka wapelekwe kwenye vyombo vya sheria lakini pia mifuko ya mikopo ni midogo kulingana na wahitaji.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamaishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyevaa miwani) na timu aliyoongozana nayo wakitoka katika ofisi za SIDO

Tangu kuanza kwa shirika hilo mafanikio yaliyopatikana nai pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Mtaa, Halmashauri hadi Mkoa lakini pia watoa ombi kwa Halmashauri kutenga maeneo kwaajili ya wajasiriamali na kuwapa nafasi za kuuza samani katika ofisi zao. 

No comments:

Post a Comment