Sunday, June 19, 2016

Mkuu wa Mkoa asikiliza changamoto za Wafugaji wa Nkasi na kuahidi kuzifanyia kazi.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameahidi kufanyia kazi changamoto na kero zote walizonazo umoja wa wafugaji katika Halmashauri ya wilaya ya Nkasi alipohudhuria katika kikao chao kinachofayika kila mwaka mara moja.

aliyasema hayo baada kusikiliza risala ndefu iliyosomwa na katibu wa umoja huo Jisena Bilia katika ukumbi wa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwatoa hofu wafugajijuu ya kero zao na kuwaomba wampe ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha malengo yanafikiwa na maendeleo yanapatikana.

Wafugaji wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Mkoa katika Mkutano.

Wafugaji wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Mkoa katika Mkutano.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwatajia wafugaji hao namba yake ya simu kwa yeyote mwenyeshida ambayo inahitaji msaada wake atakuwa tayari kutoa ushirikiano ili kutatua matatizo yao.

Katibu wa Umoja wa Wafugaji katika Wilaya ya Nkasi Jisena Bilia akisoma risala waliyoiandaa kwa Mkuu wa Mkoa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika mkutano wao wa kila mwaka Wilayani nkasi.

 Sehemu ya Risala.

Wilaya ya Nkasi ina wafugaji 5,884 wanaojihusisha na ufugaji wa ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kwa sasa wilaya inakadiriwa kuwa na ng’ombe 107,854. Idadi ya wafugaji bora ni 1,079, idadi ya ng’ombe bora ni 33,500wenye thamani ya Tsh. Bilioni 23.5. Aina ya Uzao wa ng’ombe ni Santa gertruids (kutoka Afrika Kusini), Simmental (kutoka Ujerumani) Boran, Friesian, Ng’ombe wa Ufipa (Ufipa Breed) zebu na Ng’ombe wa Asili (TZ)

Umoja huu ulianzishwa tarehe 07/02/2013 na kusajiliwa Tarehe 30/09/2013 ambapo ulianza na wanachama 160 na hadi una wanachama 230. Umoja huu ullianzishwa kwa kufuata sera ya Taifa ya mifugo mwaka 2006 ambayo  madhumuni yake ni kuongeza uzalishaji wa nyama bora inayokidhi viwango vya soko la ndani nan je ili kuongeza kipato cha wafugaji hatimaye kuboresha hali zetu za maisha.

Umoja huo ulimuelezea Mkuu wa Mkoa juu ya malengo ya kuanzishwa kwake, miongoni mwa hayo malengo ni kuwaunganisha wafugaji,kuboresha ufugaji unaoendana na mazingira, Kuimarisha uhusiano baina ya wafugaji na wakulima,  Kuhamasisha wafugaji kufuga ng’ombe wachache, kwa kisasa na kulingana na maeneo ya malisho. Kuwasaidia wafugaji kupata masoko na madawa kwa urahisi, Kudhibiti ukorofi na uhamiaji holela wa wafugaji na kusaidia kuendeleza sera ya Taifa ya mifugo

Na miongoni mwa mafanikio waliyoyapata ni Kuwaunganisha wafugaji 230 na kuwashawishi kununua ng’ombe wa kisasa na kufuga kisasa.  Kuweza kuimarisha uhusiano na taasisi mbalimbali pamoja na kupunguza migogoro baina ya wafugaji na wakulima kwa kushirikiana na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Nkasi (MVIWATA) pia Viongozi wa Umoja kuweza kuhudhuria kongamano Zaidi ya 34 nchini nan je ya nchi, pia kushinda mashindano kadhaa

Mbali na kumueleza Mkuu wa Mkoa mafanikio lakini pia walionesha kuwa na matarajio ya kuweza kuwafikisha mbali zaidi na kati ya hayo ni  Kuendelea kuwashawishi wafugaji kujiunga na umoja huo na kufuga kisasa ili kuwa na ufugaji bora. Kuwahamasisha wafugaji kuwa na makazi bora na kuondokana na tabia ya kuhamahama ili kuweza kuwapeleka watoto wao wakasome shule na kuwazuia kuwaozesha watoto wao wa kike katika umri mdogo.  Kumiliki machinjio ya kisasa, majosho na minada inayomilikiwa na wafugaji na kuendelea kuimarisha mahusiano na wakulima na  Kuanzisha SACCOS

Lakini kila penye mafanikio hapakosi changamoto, hivyo hawakusahau umuelezea Mkuu wa Mkoa Changamoto na shida mbali mbali wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na Upungufu wa majosho na mafisa ugani wa mifugo katika ngazi za vijiji na kata  Kutokuwa na maeneo tengefu ya malisho na soko la uhakika la mifugo na mazao yake na  Masharti magumu ya taasisi za kifedha katika kuwakopesha wafugaji.

Hivyo waliiomba serikali kupitia Mkuu wa Mkoa kuwasadia Kuongeza madawa kwenye madawa ya mifugo na kuona uwezekano wa kuanzisha benki ya wafugaji ili kuondokana na masharti magumu ya taasisi za kifedha. Kutafuta masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi. Kukiwezesha iwada cha nyama cha SAAFI kilichopo Sumbawanga kiweze kununua Ng’ombe.

No comments:

Post a Comment