Sunday, June 19, 2016

Mkuu wa Mkoa atembelea uwanja wa ndege wa muwekezaji katika kijiji cha Kipili


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen baada ya kuwasili katika kiwanja kidogo cha ndege kinachotumiwa na wawekezaji katika kijiji cha Kipili, Wilayani Nkasi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi akipata maelezo juu ya matumizi ya kiwanja hicho kidogo cha Ndege kinachotumiwa na Wawekezaji katika kijiji cha Kipili, Wilayani Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Iddi Kimanta (wa pili kutoka kushoto) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Julius Mseleche (wa tatu kutoka kushoto) na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyolinda mipaka ya nchi na usalama wa raia ziwa Tanganyika wakimpa maelezo Mh. Mkuu wa mkoa juu ya historia ya Uwanja huo.

No comments:

Post a Comment