Monday, June 20, 2016

Mkuu wa Mkoa atembelea wawekezaji katika kijiji cha Kipili, wilayani Nkasi

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen pamoja na Mh. Iddi Kimanta mkuu wa Wilaya ya Nkasi wakiwasili Lakeshore Lodge wakitokea Lupita Island Lodge. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ametembelea miradi ya wawekezaji iliyopo atika Kijiji cha Kipili ili kujua changamoto mbali mbali wanazozipata wawekezaji hao katika kukuza pato la taifa hasa katika sekta ya Utalii.

Kijiji cha Kipili Wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa kinasifika kwa kuwa na Miongoni mwa Nyumba ghali za kulala wageni hapa nchini kwetu inayoitwa Lupita Island Lodge, iliyopo katika kisiwa ndani ya ziwa Tanganyika ambapo kwa usiku mmoja hulipia dola za kimarekani kuanzia 800 hadi1000 ambazo ni sawa na fedha za kitanzania Milioni 1.7 hadi Milioni 2.1 (kwa chenji ya 1$ = Tsh. 2,193) na kuweza kuhudumiwa vinywaji na vyakula utakavyohitaji kwa bei hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiongea na Mkurugenzi wa Lupita Island Lodge Belinda Lightow 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akivalishwa life jacket na mmoja wa afisa usalama wa Jeshi la Wananchi ili kujitayarisha kwenda Lupita Island Lodge kuona uwekezaji.

Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Iddi Kimanta akimtambulisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen kwa Mkurugenzi wa Lupita Island Lodge Belinda Lightow kabla ya kupanda boti na kuelekea kwenye kisiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisalimiana na Meneja msaidizi wa Lupita island Lodge Shabani Kipenzi mara tu baada ya Kuwasili katika kisiwa hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa amepanda kigari maaluma tayari kuelekea kwenye Lodge 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimaliza maongezi na Mkurugenzi wa Lupita Island Lodge Belinda Lightow 


Baada ya Kutoka Lupita Island Logde, Mkuu wa Mkoa alimalizia ziara yake Lake shore Lodge iliyopo pembezoni mwa Ziwa Tangayika, ambapo kwa usiku mmoja unallipia Dola za Kimarekani 40 kwa mtanzania na 80 kwa mgeni, bila ya Chakula wala Vinywaji, kama utahitaji chakula na vinywaji kwa mtanzania utalipa Dola za kimaekani 75.Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiagana na  Mkurugenzi wa Lupita Island Lodge Belinda Lightow 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisalimiana na Mkurugenzi wa Lakeshore Lodge Selina Hofall alipowasili katika Lodge hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (katikati)akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Lakeshore Lodge Selina Hofall alipowasili katika Lodge hiyo. Kulia ni Mh. Iddi Kimanta mkuu wa Wilaya ya Nkasi akiwa maeungana kwenye msafara na kusubiri maagizo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Lakeshore Lodge Selina Hofall changamoto wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na miundombinu ya barabara kutoridhisha. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiagana na wafanyakazi wa Lakeshore Lodge. kulia Mkuu wa wilaya ya Nkasi Mh. Iddi Kimanta akiagana na Mkurugenzi wa Lakeshore Lodge Selina Hofall

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiagana na timu ya maafisa wa usalama pamoja na serikali ya kijiji alioongozana nayo katika kuangalia uwekezaji wa utalii katika kijiji cha kipili.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiandika maoni yake katika kitabu cha wageni kabla ya kuanza safari ya kurudi Nkasi Mjini.

No comments:

Post a Comment