Saturday, June 18, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aahidi kuandika Barua ya Shukrani kwa yeyote atakaechangia Madawati.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiongea kwa uchungu juu ya umuhimu wa kuhakikisha wananfunzi wote katika Mkoa wa Rukwa wanakaa kwenye madawati kabla ya Tarehe 30 June. ili kutekeleza agizo la Rais.

Kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli la kutaka kila Mkuu wa Mkoa nchini kuhakikisha wananfunzi waliomo mkoani kwake hawakai chini, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen alifanya ziara ya Kuzindua ugawaji wa madawati kwa awamu y pili katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.

Halmashauri hiyo ina jumla ya shule za msingi za serikali 103 zenye upungufu wa madawati 5464 sawa na asilimia 35 ya jumla ya madawati 15600, na shule za Sekondari 22 zenye upungufu wa meza na viti 1702 sawa na asilimia 26 ya jumla ya meza na viti 4765.

Katika Uzinduzi huo madawati 2450 kwa shule za msingi pamoja na viti 700 na meza 700 kwa shule za Sekondari yalikuwa tayari kugawiwa mashuleni na kufanya awamu zote mbili kuwa na idadi ya madawati 4087  na kufikia asilimia 91 ya uamilifu wa zoezi hilo na viti 1231na Meza 1231 na kufikia asilimia 92 ya ukamilifu wa zoezi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Julius Mseleche ameahidi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuwa kabla ya kufikia tarehe 30 June, 2016 atamualika tena kwenda kuzindua madawati kwa awamu ya tatu ili kumalizia upungufu wa asilimia 9 kwa shule za Msingi na asilimia 8 kwa shule za Sekondari katika Halmashauri hiyo.

Kamishna Mstaafu Zelote Stephen hakuacha kusisitiza kuwa kumaliza tatizo la madawati kusiwe mwisho wa matatizo, na kuamuru kuwa mbao zitakazobakia zielekezwe kwenye kupaua madarasa mbalimbali ambayo hayajaezekwa.

"Mbao hizo zisiishie kwenye madawati bali pia kupaua madarasana vyoo ili kuboresha mazingira ya usomi na elimu kwa watoto wetu" Mkuu wa Mkoa alisema.

Mkuu wa Mkoa aliongeza kuwa "ili kuonesha thamani ya mchango wa kila mwananchi aliyesababisha zoezi hili kufanikiwa basi aandikiwe barua rasmi ya shukrani nami niko tayari kuweka saini yangu" aliyatoa maagizo hayo kwa Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mh. Iddi Kimanti.

Kwa kipidi chote cha utengenezaji wa Madawati, Viti pamoja na Meza Wilaya ya Nkasi imekuwa na vituo vitano ambavyo ni Kilangala Vocational Training Center, Nkana, Msakatonge, Isunta pamoja na RS woodworks, vyenye mafundi zaidi ya 90  kwaajili ya kutengeneza madawati.

Katika kuhakikisha Halmashauri hiyo inafanikiwa kumaliza upungufu huo, iliwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo watu binafsi waliotoa madebe na magunia ya mahindi na maharage kwaajili chakula cha mafundi, pia serikali za vijiji mbalimbali ziliweza kutoa miti na mbao kadhaa wafanyabiashara na TANAPA walitoa Milioni 18 zilizosaidia kutengeneza Viti 461 na Meza 461, na Jeshi la Wananchi Tanzania kutoa gari 2 kwaajili ya Kusambazia madawati mashuleni.

Tarehe 9 May,2016 Kamishna Mstaafu Zelote Stephen aliweza kufika katika Halmashauri hiyo na kufanya uzinduzi wa Awamu ya kwanza ambapo alizindua ugawaji wa madawati 1637 na meza na viti 531.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen wa katikati akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Iddi kimanta (mwenye shati ya kitenge) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Julius Mseleche (wa kwanza kulia)

Mwenyekiti wa Kamati ya madawati katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Emanuel Kushoka akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaaafu Zelote Stephen katika kuwapongeza wale wote waliochangia kufanikisha zoezi la utengenezaji wa madawati katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Mwakilishi wa Jeshi la Wananchi Tanzania Ali Omar akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaaafu Zelote Stephen katika kuwapongeza wale wote waliochangia kufanikisha zoezi la utengenezaji wa madawati katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Mwakilishi wa Wakala wa Huduma za misitu, Protas Karia akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaaafu Zelote Stephen katika kuwapongeza wale wote waliochangia kufanikisha zoezi la utengenezaji wa madawati katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Mwakilishi wa Renatus Mahombwe aliyechangia madawati 30 akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaaafu Zelote Stephen katika kuwapongeza wale wote waliochangia kufanikisha zoezi la utengenezaji wa madawati katika Halmashauri ya Wilaya ya NkasiMkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Iddi Kimanta nae katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa hakuacha kuunga Mkono juhudi za wananchi, nae alichangia debe 3 za maharage pamoja na Ofisi yake kutoa miti kadhaa waajili ya mbao. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Julius Mseleche akisoma taarifa ya utengenezaji wa madawati wa awamu ya pili mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyeshika kiuno) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Iddi Kimanta (kusliani kwake) na mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Julius Mseleche (kushotoni kwake) wakiangalia baadhi ya magogo yaliyotolewa kama mchango na wananchi na Taasisi mbalimbali kwaajili ya kuchania mbao za madawati, viti na Meza.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisalimiana na baadhi ya wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi wakati alipowasili.

Baadhi ya Madawati yaliyokuwepo kwenye uwanja wa kituo cha RS woodwork Katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambapo Uzinduzi huo Ulifanyika

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitembelea maeneo tofauti kuona matengenezo ya Madawati, viti pamoja na meza vikitengenezwa.

Baadhi ya Madawati yaliyokuwepo kwenye uwanja wa kituo cha RS woodwork Katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambapo Uzinduzi huo Ulifanyika

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa amepozi kwaajili ya picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa RS woodwork ambao wameacha shughuli nyingine zote na kutenga muda wao kwaajili ya kuhakikisha mpaka kufikia tarehe 30 June,2016 wanakamilisha madawati yanayohitajika ili wananfunzi katika Wilaya ya Nkasi wasikae chini.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitaniana na baadhi ya wafanyakazi wa RS woow works 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa amepozi kwaajili ya picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa RS woodwork ambao wameacha shughuli nyingine zote na kutenga muda wao kwaajili ya kuhakikisha mpaka kufikia tarehe 30 June,2016 wanakamilisha madawati yanayohitajika ili wananfunzi katika Wilaya ya Nkasi wasikae chini.

Wafanyakazi wa Idara mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi wakiendelea Kumsikiliza mkuu wa Mkoa akitoa pongezi kwao.

Baadhi ya Magogo yaliyokuwepo kwenye uwanja wa kituo cha RS woodwork Katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambapo Uzinduzi huo Ulifanyika

Baadhi ya Madawati yaliyokuwepo kwenye uwanja wa kituo cha RS woodwork Katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambapo Uzinduzi huo Ulifanyika

No comments:

Post a Comment