Friday, June 17, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa atembelea Kituo maalum cha Kutengezea madawati wilaya ya Nkasi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisaini kitabu cha wageni katika moja ya dawati la shule ya Msingi kuona ubora wake. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisaidia kushika mbao inayokatwa kwaajili ya kutengeneza madawati katika kituo cha Ufundi Malangali (Malangali Vocational Training) kilichopo wilayani Nkasi,Rukwa. kushoto kwake ni Mkuu wa Kilangala Mission,Moses Siyame 

Kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli la kuhakikisha kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati au kiti ifikapo tarehe 30 mwezi wa Sita mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen alitembelea moja ya vituo vitano vinavyotengeneza madawati katika Wilaya ya Nkasi ili kuona maendeleo ya zoezi hilo.

Kituo hicho mbali na shughuli za kimasomo pia kimetenga muda wa kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa ambapo kabla ya tarehe 30 June kinachotarajia kutengeneza madawati 500 ya Shule za Msingi pamoja na viti na meza 400 kwa shule za Sekondari.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiangalia ujenzi wa madawati katika kituo cha Ufundi Malangali (Malangali Vocational Training) kilichopo wilayani Nkasi,Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akikagua madawati ambayo yameshatengenezwa katika stoo ya kituo hicho cha Ufundi Malangali (Malangali Vocational Training) kilichopo wilayani Nkasi,Rukwa. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mh. Iddi Kimanta na wa katikati ni Mkuu wa mission Malangali, Moses Siyame.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimsisitizia Mkuu wa Mission Malangali, Moses Siyame kuongeza wafanyakazi wengi zaidi ili zoezi liende haraka iwezekanavyo. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh, Iddi Kimanta (kuliani mwa mkuu wa mkoa) Afisa elimu Mkoa, Khalfan Masukira (aliyeshika Daftari) a Mkuu wa Malagali Mission Moses Siyame (mwenye Flana ya Mistari)


No comments:

Post a Comment