Friday, June 17, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amtembelea Mwenyekiti wa Kitongoji kujua kero

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amemtembelea      Mwenyekiti wa kitongoji cha Kipili, Filbert Patrick Kilala katika Kijiji cha kipili, wilayani Nkasi ili kufahamu kero mbalimbali anazozipata ikiwemo za wawekezaji katika kitongoji hicho.

Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika msafara huo alikuwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Iddi Kimanti pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi, Julius Mseleche.

Mkuu wa Mkoa kabla ya Kuingia nyumbani kwa Mwenyekiti wa kitongoji hicho alionana na Mwenyekiti wa kijiji ili amkutanishe na mwenyekiti wa kitongoji kuweza kuzungumza pamoja. 

Mwenyekiti huyo alistaajabu kuona Mwenyekiti wa Kijiji hicho Dakus Kambega amekaa sebuleni kwake, na watu ambao hakuonesha kuwafamu na baada ya kuulizwa alikuwa muwazi na kusema hakuna anaemfahamu, ndipo alipotambulishwa na kuendelea na maongezi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akimuuliza maswali Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kipili, Wilayani Nkasi, Filbert Kilala juu ya kero zinazomsibu katika kitongoji Hicho. (kwenye kochi la mtu mmoja ni Dakus Kambenga, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipili)


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Iddi Kimanti (kushoto) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Julius Mseleche (aliyevaa suti nyeusi) wakiendelea na mazungumzo nyumbani kwa Mwenyekiti wa Kitongoji, Filbert Kilala (aliyesimama) pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji Dakus Kambenga 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoka nyumbani mwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kipili, Wilayani Nkasi.

No comments:

Post a Comment