Thursday, June 23, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa asisitiza ushirikiano na wafanyabiashara katika kuujega Mkoa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwatoa wasiwasi wafanyaboiashara juu ya kupatikana kwake kwa yeyote atakayetaka washirikiane kuijenga Rukwa. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TCCIA Sadrick Ikuwo na Kudhotoni kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Mathew Sedoyyeka.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewaomba wafanyabiashara wa Mkoa wa Rukwa Kumpa ushirikiano wa Kutosha ili kuweza kuijenga Rukwa kwa manufaa ya Vizazi vijavyo.

Ameyasema hayo katika kikao maalum cha wafanyabiashara na wajasiriamali wa Mkoa wa Rukwa kilichoitishwa na Mwenyekiti wa Tanzannia Chember of Commerce Indusry and Agriculrure (TCCIA) Sadrick Ikuwo katika ukumbi wa Libori katika Manispaa ya Sumbawanga. 
 “Mimi niko Zaidi ya Tayari kushirikiana na yinyi” Mkuu wa Mkoa alisema kwa Kusisitiza
“Mkuu wa mkoa aliyepita Mh. Saidi Magalula alinigusia kitu hiki na akanihusia niendelee kukilea” aliendelea kusema. 
Kamishna Mstaafu Zelote Stephen hakuacha kuwatadharisha wafanyabiashara kufuata sheria katika kuendesha biashara zao kwa kukazia kuwa kila kitu kina utaratibu wake na kuwa nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria.

“kila kitu kina utaratibu wake n ahata mpira unataratibu zake na sheria zake, kuna penalty, kuna offside, ukifanya makosa kuna kadi ya njano na kama ukifanya madhambi makubwa kuna nyekundu ambayo inakutoa nje ya uwanja kabisa, hivyo tuzitafute Sheria, Tuziheshimu na tuzitumie”

Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa hakusita kuwatahadharisha wafanyabiashara kuachana na kuuza bidhaa feki na pia kuwahudumia wateja kwa lugha nzuri ili kuweza kuongeza wateja kwenye maeneo yao ya kazi.

“Naona swala la mbegu feki linapigiwa sana kelele, hili achene lakini pia na bidhaa zote nyingine kama madawa ya binaadamu nakadhalika pia sio jambo la busara kuuza bidhaa feki, hivyo mtu asitegemee kuuza mbegu feki halafu tukamwachia kisa akiulizwa anasema ndio anaanza kutafuta maisha, hatuwtamsamehe mtu kama huyu ambae atatuzalishia masikini wengi zaidi”

Mkuu wa Mkoa aliongeza kuwa kwa kupitia TCCIA pekee ndio itaweza kuwainua wafanyabiashara, wakomae na kutodumaa na kuitegemea TCCIA kuwa kichocheo cha biashara na uwezeshaji.

“Tunataka TCCIA iwe ndio Think Tank a isitumike kulaumu tu maana ikiwa hivyo hakutakuwa na viwanda wala maendeleo, nyenzo pekee za kimaedeleo ni kujenga mahusiano mazuri, kushirikiana na kuelimishana ili wote tuweze kusonga mbele kwa pamoja”
Mwakilishi wa EFTA kampuni inayokopesha mashine kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, ambae pia ni Meneja wa Kampuni ya Lonagro LTD inayosambaza vifaa vya JOHN DEER,  Daniel Mugittu akifafanua shughuli za EFTA kwa wafanyabiashara waliohudhuria katika kikao hicho 

Afisa Biashara wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Aman Mkandarasi akitoa taarifa fupi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga juu ya kuelezea Tozo mbalimbali za ushuru katika bishara mbalimbali na sheria zake.

Msemaji wa Jeshi la Zima Moto na uokoaji Mkoa wa Rukwa, Chesco Mbata akifafanua hatua mbalimbali zinazotakiwa kuchukuliwa ili kjiepusha na majanga ya moto katika maeneo ya biashara pamoja na makazi ya watu na maeneo ya mahospitali na kumbi za starehe katika Mkutao wa wafanyabiashara wa Mkoa wa Rukwa.

Baadhi ya Wafanyabiashara na watumishi wa idara na taasisi za serikali waliohudhuria Mkutano huo.

Baadhi ya wafanyabiashara mbalimbali waliohudhuria kwenye kikao.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (aliyeweka peni mdomoi) akisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika Mkutano wa Wafanyabiashara wa mkoa wa Rukwa.

Mwenyekiti wa TCCIA Sadrick Ikuwo akiwaomba wafanyabiashara wenzake kumpa ushirikiano mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen katika kuukuza Mkoa wa Rukwa Kibiashara lakini pia katika kuunga mkono agizo la Rais juu ya suala la madawati.

Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Mathew Sedoyyeka (aliyesimama)  akisisitiza usafi kwenye maeneo ambayo wafanyabiashara hao  wanapatia riziki zao ili wasije kuiona serikali mbaya pindi itakapokuwa inatekeleza sheria zake. lakini pia Hakusita kuwakumbusha wanaRukwa kuendelea kupanda miti ili kutunza mazingira lakini pia kujipatia utajiri.

Mwakilishi wa Meneja na pia ni Afisa biashara wa Shirika la viwanda vidogovidogo SIDO Mkoani Rukwa Salome Charles (aliyesimama) akielezea kzi na mipango mbalimbali ya SIDO katika Mkoa wa Rukwa kwenye Mkutano wa Wafanyabiara wa Mkoa wa Rukwa. 

No comments:

Post a Comment