Sunday, June 19, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa atembelea mabwawa ya Samaki Zanzibar

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amepongeza kitendo cha vijana wawili wa kitongoji cha Zanzibar katika Kijiji cha Katumba Azimio, katika Manispaa ya Sumbawanga kuwekeza katika ufugaji wa samaki.

Vijana hao Emaueli Lymo na mwenzie Musa Daudi wana mabwawa kumi yenye ukubwa wa robo eka kwa kila bwawa na yenye uwezo wa kuzalisha samaki 44,630 wa saizi ndogo, Kati na kubwa wenye thamani ya Shilingi Milioni 38. Samaki wanaopatika hapo ni Kambare na jamii ya Sato.

Mradi huo wenye lengo la kuwanufaisha wananchi kupitia ajira, kuwa kituo cha usambazaji samaki na kutoa elimu ya ufugaji wa samaki kwa jamii, wakati mradi huo unaanzishwa tarehe 4, May, 2015 uligharimu shilingi Milioni 16.5 ukiwa na jumla ya vifaranga vya samaki 4,500.

Kamishna Mstaafu baada tu ya kusikia juhudi za vijana hao alishikwa na hamu ya wenda kuona mendelo yao na kuweza kuwasaidia pale watakapohitaji msaada wake na kuwasisitiza vijana hao kuwashawishi vijana wenzao kujiunga na mradi huo na kuacha kulala na kucheza “pool table” mchana kutwa.

“Nawaomba muwashawishi vijana wenzenu ili kuwe na miradi mingi ya namna hii kuliko kucheza pool table na kulala” Mkuu wa Mkoa alisema.

Na kuongeza kuwa kadiri wanavyozidi kwenda mbele ndipo wanapojifunza Zaidi lakini pia wasisahau kushirikiana na wataalamu ambao wapo chini yake ili kuweza kupata mafanikio ya uhakika na kuboresha huduma zao.

Vijana hao pia hawakusahau kuwashukuru maafisa uvuvi Bakari Saidi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga pamoja na Johaness Kabakama kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano wao wa ushauri wanaowapatia mara kwa mara katika kufanikisha mradi huo.


Pia vijana hao waliwashukuru wananchi wa kijiji cha Katumba Azimio kwa usirikiano wao wanaowapa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwanasihi vijana wenye mradi wa kufuga samaki kuwashawishi na wenzao ili kujikwamua katika umasikini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akisikiliza Risala iliyosomwa na kijana mwenye mradi huo Musa Daudi mbele ya wanachi na serikali ya kijiji cha Katumba azimio.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akionyeshwa aina mbalimbali za mabwawa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen na timu aliyofuatana nayo wakipita katikati ya matuta yanayotenga mabwawa ya mradi huo.

Wavuvi wa mabwawa hayo wakimuonesha Mkuu wa Mkoa namna wanavyovua na aina ya samaki waliomo kwenye mabwawa hayo

Wavuvi wakionesha baadhi ya samaki waliowavua Mbele ya mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwabembeleza wanachi kuwatumia wataalamu waliopo kwenye ofisi yake kwa manufaa yao wenyewe.

No comments:

Post a Comment