Thursday, June 23, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa awaomba Viongozi wa Dini kuzidi kuomba amani

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (wa katikati waliokaa) akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi mbalimbali wa Dini katika Mkoa wa Rukwa.  wa kwanza kushoto waliokaa ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Mathew Sedoyyeka.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwaomba viongozi wa Dini kuendelea kuomba amani katika Mkoa wa Rukwa katika Mkutano maalum alioutisha katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano katika ofisi za Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewaomba Viongozi mbalimbali wa Dini wa Mkoa wa Rukwa Kuzidi kuomba amani katika Mkoa huu ili wananchi waweze kufanya shughuli za kimaendeleo bila ya Buguza na kusisitiza kuwa wao kwa wao waweze kushirikiana katika kuitunza amani.

 “Nawaomba mzidi kuomba Amani yetu iwe kubwa” Mkuu wa Mkoa alisema katika Mkutano alioufanya na viongozi hao katika ukumbi mkubwa wa ofisi za Mkoa wa Rukwa. 

Kamishna Zelote Stephen alifafanua kuwa Viongozi wa Dini ni silaha yenye nguvu sana katika kutunza amani ya mahala popote pale nchini na kwamba wao ndio wanaowatengeneza wananchi wenye kuheshimu misingi na sheria za nchi kwa kuwapa elimu mbalimbali katika kujenga imani zao.

Mkuu wa Mkoa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen hakusahau kuwasisitiza kuwapa ushirikiano pale watakapouhitaji na kuwa yeye haitaji "appointment" ili kuonana nae. 

“Muda wowote unapotaka kuzungumza na mimi, karibu sana, huna haja ya kuonana na msaidizi wangu ili akupangie appointment, kwangu mimi hapana, kwasababu unaweza ukaja na jambo sijui ni la nini halafu nikwambie uje baadae! Hapana” Mkuu wa Mkoa alisema.

Baadhi ya Viongozi wa Dini waliohudhuria katika mkutano huo.

Baadhi ya Viongozi wa Dini waliohudhuria katika mkutano huo.

  Mtumishi Charles Mujuni Magebe akiiiomba serikali kwa kuwatumia wataalamu wake waweze kuendelea kuwaelimisha wananchi  juu ya upandaji wa Miti ili kuuokoa Mkoa wetu na kulinda mazingira ya Mkoa Lakini pia hakusita kuzungumzia tatizo la wafugaji wengi kuchunga mifugo yao bila ya mpangilio maalum na kusababisha migongano baina ya wafugaji na wakulima.

         Askofu Henry Tadayo Chomoya – katibu AIGT Aomba viongozi wa dini washirikishwe katika vikao mbalimbali vya maendeleo kama vile WDC kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa. Pia aliwasihi watendaji mbalimbali pamoja na watumishi wenzao kuheshimiana kiimani na katika kutenda majukumu mbalimbali.

        Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Rashid akilimali akiitahadharisha Serikali Kutokana na kusambaa kwa mbegu feki na kuiomba serikali kusambaza mbegu bora vijijini ili wakulima waweze kuinua kipato chao cha maisha kwani wananchi wanapata shida sana na wingi wa mbegu feki.

Tatizo la ardhi nalo hakusita kuligusia pale aliposema kuwa katika Manispaa ardhi imekuwa ndogo na hivyo watendaji wanapeana wao kwa wao na kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen Zelote Kuliangalia Jambo hilo kwa umakini wa hali ya juu.

Akiunganisha katika hilo pia alizungumzia pingamizi zinazojitokeza katika maeneno mbalimbali pindi waislamu wanapotaka kujenga Misikiti.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwa na Kaimu RAS Mka wa Rukwa Abubakar Kunenge, walipokuwa wakitoa takwimu za wafanyakazi hewa na kuwaahidi viongozi hao wa Dini kuwa atawashughulikia wafanyakazi wote wababaishaji katika Mkoa wa Rukwa ili kubaki na wafanyakazi makini wenye kupenda maendeleo.

Katika Taarifa fupi hiyo. Kaimu Katibu Tawala Abubakar Kunenge alisema kuwa Tangu mwaka 2013 hadi mwezi May mwaka 2016 tayari wafanyakazi hewa 647 wamebainika huku ikiwa 492 walikuwepo kabla ya Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Magufuli kuingia madarakani.

Baadhi ya Viongozi wa Dini wakijitayarisha kupiga picha ya Pamoja 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (wa katikati waliokaa) akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Rukwa. wa Mwanzo kushoto waliokaa ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Mathew Sedoyyeka.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (wa katikati waliokaa) akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Dini wa Mkoa wa Rukwa. wa Mwanzo kushoto waliokaa ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mh. Mathew Sedoyyeka. 

No comments:

Post a Comment