Sunday, June 19, 2016

Mkuu wa mkoa wa Rukwa awaomba wafanyakazi wa Afya kuwaripoti wafanyakazi bandia wa sekta hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa nasaha zake katika kikao cha kazi cha Wasimamizi wakuu wa Zahanati na Vituo vya Afya 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akiwatahadharisha  Wasimamizi wakuu wa Zahanati na Vituo vya Afya kutoa taarifa pale wanapobaini kuwa kuna wafanyakazi wasio na sifa katika maeneo yao ya kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen, amewataka wasimamizi wakuu wa zahanati pamoja na vituo vya Afya kutekeleza mafunzo wanayoyapa kwa vitendo ili kuboresha huduma za afya katika Wilaya ya Nkasi.
Aliyasema hayo katika kikao kifupi cha kazi cha watumishi hao wa afya kikao kilichounganishwa na mafunzo ya mradi wa afya za msingi ziwa Tanganyika (Kipili Health Project) alipofanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ili kujua maendeleo ya Halmashauri hiyo katika sekta mbalimbali.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kukumbushana majukumu mbalimbali ikiwemo Chanjo Mkoba, Utawala na usajili wa CHF kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkansi Mh. Iddi kimanta pamoja na
Kamishna Mstaafu Zelote aliwasisitia kuwa taifa letu haliwezi kujengeka kama wananchi wake watakuwa na afya mgogoro na kuongeza kuwa mafunzo wanayoyapata yawatawale nan a kushikamana nayo.

Mkuu wa Mkoa hakusita kuwatahadharisha wasimamizi hao juu ya kuwaripoti wafanyakazi wote ambao hawna sifa ya kufanya kazi hizo ili kupunguza hatari ya kutoa huduma mbovu na kuwafanya wananchi kupoteza Imani na watumishi wa afya katika Wilaya ya Nkasi.

“Kama kuna wahudumu wa afya ambao hawana sifa, tafadhalini toeni taarifa mapema, ni heri kuwa na mhudumu mmoja mwenye sifa kuliko kuwa na mia moja wasio na sifa ambao wanaweka afya za wananchi hatarini” alisema Mkuu wa Mkoa.

Kamoshna Mstaafu pia Aligusia Suala la usafi katika Zahanati na ushawishi wa wananchi kujiunga na CHF, alisema “Zahanati nyingi ni chafu, hata ule usafi wa kawaida inashindikana na zahanati nyingine zinatelekezwa kabisaa na pia wananchi wanakata tamaa kujiunga na CHF kwakuwa huduma zinazotolewa haziridhishi”


Pia hakuacha kuzungumzia suala la upotevu wa madawa katika zahanati hizo na kutowashirikisha kamati za afya vijijini (CHMT) na kuonesha kusikitishwa na vitendo hivyo, na kusisitiza matumizi ya macshine za kukatia risiti ili kuongeza mapato katika Halmashauri hiyo. 

Wasimamizi wakuu wa Zahanati na vituo vya afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi waliohudhuria kwenye kikao 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akitoa mawasiliano kumpa Bi. Marjo Tenkate, Mshauri wa mradi wa Afya za Msingi ziwa Tanganyika (Kipili Health Project) mradi unaofadhiliwa na watu wa Denmark, Kanisa la Monravian kutoa makazi kwa watumishi na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kutoa watumishi. wa katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Julius Mseleche
Bi Joyce Malambika akionesha Mchoro wa kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais wa Nchi yetu Dk John Pombe Magufuli wa "Hapa kazi tu" katika namna ya pekee.

No comments:

Post a Comment